Wednesday, May 9, 2012

BONGO DARISALAMA, PAMOJA NA KADHIA YA KERO ZAKE PIA INA UNAFUU WAKE

Haki ya nani Ulimwengu una mambo yake,
na misemo yake kibao.
Utasikia
Ukiristo mgumu........
Uislamu mgumu............
Ujamaa mgumu.................
ama kweli
Na Bongo Darisalama nayo ngumu.
Mpaka Blogger anafikiria kuikimbia ifikapo 2020.
Lakini Bongo Darisalama si ngumu tunavyoiona wakati mwingine.....KAZI
Ukifanya kazi, Bongo Darisalama maisha yanaenda.
Dada ananunua vocha Zantel kwa mia 200, anabahatisha kuuza Special Numbers, akikupatia Tshs 1,800 zimeingia mfukoni, maisha yanaendelea
 Rafiki yangu mhaya, mtaalamu wa ushoni wa kuripea viatu, na ziada ya kukusanya chupa tupu za plastic, maisha yanaendelea pamoja na ulemavu wake. Na mchana si haba kumkuta AfriCentre akipata Safari moja ya moto na moja ya Baridi, na siku imepita.
Babu kwa kukusanya chupa tupu, hapa nilimkuta mitaa ya keko maliasili
 Bendera za timu za mpira, au za nchi mbalimbali zinamweka mjini mheshimiwa huyu
Reflectors za magari, Triangles, Jeki nk. hata kama hauzi kila siku
life goose on
Perfumes na airrefreshner, mitaa ya machinga complex Kawawa Rd
Benki za simu, MPESA, TIGO PESA, zote zinalipa
Mtaji wako unatosheleza? unayo leseni?
Bodaboda halali yako hata kama umejifunza asubuhi na jioni ukabeba abiria.
Bongo maisha yanaendelea

1 comment:

  1. kweli kuhangaika kwa njia hizi ni bora kuliko kuiba. kazi ni kazi .......

    ReplyDelete