Thursday, December 15, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - FINAL LAP

Final Lap ya vacation yangu inaanza Jumatatu 24/10 Alfajiri Mwanza. Tofauti na wakati wa safari ya kuja Nakatuba, On wheel nabakia mimi pekee, no Co Driver.

Kuna Mabadiliko ya abiria pia.

Tuongozana na Mzee CK, Mama Tereza, Beria, Joshua na Nyamtakama Majira ya saa tano tunaingia Singida Town, abiria wangu inaelekea wako hoi kwa safari. Lakini tunajipa moyo, milima ya kutisha tumekwisha ipita
Stop Over Singida inatukutanisha na Dada Pendo Yoweli.
Baada ya miaka mingi namna hiyo tunapata nafasi ya kupeana kilichojili tokea wakati huo.

Break Fast yetu inakuwa hapa Singida
Chai, Chapati na maandazi
Soda kupooza koo na vijinyama choma Kilometa kama 10 hivi kutoka Singida tunapata pancha, Tunabadilisha tairi safari inaendelea.
Kilometa 35 kabla ya Manyoni pancha ingine, hatuna spare tyre.
Inalazimu kuleta tyre zote mbili Manyoni mjini.
Wajasiriamali wanachangamkia tenda hapa Manyoni

Bw Zakaria, mkamata tenda.

Baada ya hapo safari inaendelea, kilometa 45 kabla ya Dodoma tunajikuta hatuna mafuta.

Baada ya mahangaiko ya hapa na pale tunafanikiwa kupata Mafuta na kuingia Dom usiku Asubuhi Dom ninapata hizi Taswira mbili


Dom, mjini kati, na baadae safari kama kawaida

Ndani ya Kongwa Ranchi tunapata pancha ingine. Tuweka the only spare tuliyokuwa nayo


Tunafanikiwa kuwahi lunch Morogoro

Tunashare na familia ya Dr

Alasiri, Misugusugu

Barabara imefungwa kutokana na ajali ya Gari ya Dodoma iliyoua watu 23


Njia ya vichochoroni imeelemewa na magari makubwa kwa madogo

Ni watu wengi mno wako stranded

Hatimae msaada wa kuondoa gari lililofunga njia unawasili

wakihangaika kupata njia

Mkombozi wetu "BLACK MAMBA"

Na hatimae safari inaendelea

Back at Kinyerezi, saa tatu usiku Jumanne 25.10.2011


Ni furaha ilioje, kumaliza Vacation yangu Salama.

Shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa vyote

2 comments:

  1. Duh, misukosuko mmeipata. lakini bora mmefika slama. Mungu ashukuriwe kwa yote.

    asante Uncle kwa kumbukumbu hizi.

    ReplyDelete
  2. Poleni, ni zamani ila mlihangaika sana!

    ReplyDelete