Saturday, September 18, 2010

REBECCA NYAMWEYA DAY 12 DECEMBER 2010

Picha ya Nyamweya mwishoni mwa miaka ya 90 kama sikosei.
Alifariki mwaka 2002 akiwa ameshavuta zaidi ya miaka 95.
Katika kumukumbuka mtu huyu muhimu sana kwetu, na katika kujaribu kutunza kumbukumbu yake kwa kina Rebeca wajao, Mwalimu Maclaud anaandaa siku maalum ya REBECA NYAMWEYA siku ya tarehe 12.12.2010 huko KARUKEKERE.
Wajukuu wote wanatakiwa kuweko huko wakiwa na familia zao zote.
Watu wote wanashauriwa kuandaa usafiri wao binafsi, angalau kuwepo Karukekere siku moja kabla.

Kutakuwepo na kongamano na maelezo kutoka kwa watu waliokaa na Rebecca na kufahamu historia yake.
Mmepata kusikia kusikia jinsi alivyokutana na waume zake, Magoti I na Magoti II.

Nafasi yako kati ya nafasi adimu zipatikanazo kuhifadhi kumbukumbu hii.
Picha hii ilipigwa na Magoti III

1 comment:

  1. Jioni Jumamosi 11/12/2010 wageni wengi tayari walikuwa kwa Maclaud, mji ulifurika.Kamati ya maandalizi: Maclaud, Eddy, Jennifer, Mashaka, Bright, Masuruli nk ikafanya kikao cha mwisho kabisa na kufanya final touches.
    Kamati zikaundwa: chakula, ujenzi, usafiri,malazi nk
    Saa 12 asubuhi 12/12/2010 shughuli zikaanza, kila mahali pilika. Kule mjini kulikuwa na mdila
    Tisa kamili kila kitu safi, chakula kikaliwa.
    Mdau Bright kesho yake, yaani jumatatu alikuwa na mkutano dar peacock hotel asubuhi kuhusu mazingira ya bahari ya hindi, lakini saa 10 jumapili bado yuko karukekere.
    Mungu mkuu, aliweza kulala mza siku hiyo na kesho yake kuwahi kikao dar. picha zitafuata

    ReplyDelete