Total Pageviews

Monday, December 5, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - LIKIZO KWISHNEI

18.10.2011

Likizo imekwisha, safari ya kurejea inaanza.

"Pains" zinajionesha miongoni mwa watu, lakini hakuna budi kuendelea,

CK Jnr, Suzy na wengine inawawia vigumu kukubali..................................

Lakini hakuna jinsi.

Kila inapowezekana, tunapita na kuaga ndugu na jamaa

Busambara, Kibara.............. Mwl Mafuni kutoka Sunsi alikuwepo pia kutoa mkono wa kwaheri
Mwl Belly Bunda.......................Super Mteki(Bila picha ) wote wakitupa mkono wa kwaheri

"Likizo nyingine mtakapokuja badala ya kwenda mpaka huko Pida, basi mtafikia hapa"
Mzee Mwayai, Mama Nyabherenga(Nyamasisi), Mama Nyakamoga wote wakitutakia safari njema.

Saturday, December 3, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - FAREWELL DINNER

Likizo inakwisha,
Ama kweli likizo ina raha yake, natamani kuongeza siku lakini haiwezekani

Siku ya mwisho tunakaribishwa chakula cha jioni kwenye familia ya Bw Robert na Bithia
Wasindikizaji huwa hawakosekani, Kevi kama kawa tulikuwa nae

Vyombo vilifutwa hasa ilibakia kwenda kusuuza hasa,


Mdau Beria akihakikisha hakuna kinachobakia huko Joshua akiwa hoi





Mali bila daftari hupotea bila kujua,


Mdau Roba huhakikisha mali zake zote zina "reference"



Ama kweli shibe mwana Malevya...........................

Blogger hoi kwa shibe Ankal Better, Neema wakitamani nao tusiondoke

Friday, December 2, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - KANISANI KIBARA

Jumamosi 15.10.2011, Sabato. Na safari mapema alfajiri ikianzia Kibara kumchukua Mama Tereza, kumleta Nakatuba kuteta na Dadie kabla ya safari ndefu jumapili, na baadae kurudi kushiriki sabato kanisani Kibara. Njiani nikavutiwa na taswira hii ya "Sunrise" nikiwa pale kilima cha Manana, jua likitoka usawa wa kilima cha Mmagunga
Baadae ikawa nafasi njema ya kushiriki Sabato katika kanisa la Kibara, Na kupata NENO kupitia kwa Mch Kamoga.
Miaka mingi iliyopita niliposali hapa kwa mara ya mwisho nililiona kanisa hili kuwa kubwa. Lakini sivyo ilivyo leo. Haliwezi tena kutosheleza na hivyo tunalazimika kufanya ibada nje ya kanisa.

Kanisa lina mpango mzuri ambao naamini Mungu ataubariki wa kujenga kanisa lingine kwa gharama ya Tshs Million Mia mbili.
Sehemu ya sadaka yetu itaenda kugharamia ujenzi huu
Mwongozaji wa kwaya, Mafuru Mafwili akiwajibika katika kinanda

Kwaya yenye talanta ya uimbaji haswa

Wakati wa kutoka nikapata nafasi ya kutambulishwa kwa ndugu na jamaa mbalimbali ambao hatujaonana miaka mingi, miongoni mwao Mke wa Uncle Kasina
Na Mama Makuke

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - MJINI KIBARA

Welekeo ofisi ya mbunge wa jimbo la Mwibara. Ofisi hii japo sina hakika sana, itakuwemo kwenye jengo la CCM Kibara.
Mji wa Kibara una changamoto nyingi za kimaendeleo, ni mji wa muda mrefu ambao ukuaji wake umekuwa wa kusuasua. Miaka ya karibuni ulitangazwa kuwa mji mdogo. Na upimaji wa viwanja ukafanywa.

Kibara sasa inawasha stima, ingawa tatizo la maji limebakia palepele. Zamani zile tukifahamishwa ni uhaba wa mafuta ya mashine ya kusukuma maji. Leo je si kuna stima???

Jengo la CCM Kibara

Sina hakika kama kweli ni jengo la CCM au ni mali ya wananchi wote. Kwa maana zamani hizo likitumika kwa shughuli za wananchi wote. Nakumbuka 07.07.1967 tulikuwepo hapa sikukuu ya Sabasaba ukawepo ubwabwa kwa nyama ya Nyati. Kwa mahanjumati tuliyoyapata siku hiyo kesho yake nakumbuka tulirudi hapa tukidhania sikukuu inaendelea. Ni zamani sana sikumbuki tuliorudi nao siku hiyo.

Mambo ya mjini Kibara, Shalobalo Joshua mtaani
Mambo ya mjini,
Hapa ni kwa Mama Tereza
Joshua, Mama Tereza, Beria, Mama Nyasige na Nyang'oko
Chuma, Joshua, Mama Tereza, Beria na Zarau

Lake view from kwa manana

Kibara ina fukwe ndefu safi zinazofaa kwa uwekezaji wa shughuli za kitalii lakini fursa hii haijaonekana machoni pa wawekezaji.

Kibara kuna fursa ya ufugaji wa aina mbalimbali

Kwa "Nyamusarya" siyo "Msalya"

Kibara kama mji nao una vimbwanga vyake

Tuna changamoto ya stendi ya Magari ya abiria yafanyayo safari kupitia hapa

Stendi yetu Kibara

Walau sasa Kibara, kwa wale wa kilaji unaweza kupata Kili baridi, kuna sehemu chache za kupata vinywaji japokuwa hazijaanza kuchangamka kihivyo.
Tulipopata nafasi tulibadilishana mawazo kwenye vijiwe hivi.

Hapa ni Mr Jeremia aka Maradona na Shem Roba

Maradona na Ankal Suzy

Nani alisema Kibara hakuna Chips?

Ziko za kumwaga siku hizi.
Ankals Kevin, Joshua na Suzy wakithibitisha hilo siku walipotoka na Blogger

Nilikuwa nimekwisha jijengea kijiwe niwapo Kibara, na Kibara hakuna matata. Sikupata taabu ya kupata taswira hii kwani badala ya kuomba niwapige picha ilikuwa vice versa, wao waliomba niwapige picha kwa ajili ya kumbukumbu.

Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika Kibara inakabiliwa na Changamoto nyingi.

Kiwanda kilichokuwepo hapa zamani hizo kimekufa, Hospitali iliyokuwa ikitukuka nje ya mipaka ya Kibara sasa ikichechemea.........

Sidhani kama tuna haja ya kuwarudisha wahindi.

Thursday, December 1, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - KURUGONGO

KURUGONGO

MANDHARI ZA KUPENDEZA

Lakini Defostration inaendelea, na hakuna jinsi kwa sababu hakuna njia mbadala wa nishati

Mwezi na CK

CK na Kevin

Hii ndio kusenya kulikobakia, tofauti na miaka ile tuliyokuwa tukienda milima ya Magambo na Chiganga na kukusanya kuni kutoka miti na magogo iliyokufa yenyewe.


MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - MMAGUNGA VISIT

Tulipata nafasi ya kutembelea Mmagunga kuwasalimia ndugu na jamaa,
na kupata wasaa wa kubadilishana mawazo kwa hili na lile.
Hapa wazee CK na Manyama Mafwimbo nao walikuwa na yao.
Wengine humwita "Rajabu", na mie nimezoea "Ajabu"
Sina hakika nani yuko sahihi, lakini siku hii hatukuona kama kama ni muafaka kupata ufafanuzi.
Na yeye akiwa amezama katika mawazo..........pengine akiwaza
"Kuku yupi niwachinjie hawa wageni?"
Mzee Manyama na Mama Nyasige (Nyamakubhi)

Wenyeji na wageni tulikuwa wamoja ndani ya muda mfupi

CK Jnr 2 yeye hakuona umuhimu wa kuficha hisia zake wakati wowote zinapojitokeza........

Na hatimae wenyeji walituona tukiondoka

Mrs Ajabu, Nyamakubhi, Ajabu na wenyeji wengine walitusindikiza

Kutoka kwa Manyama tukapitia kwa Shemeji Bw Majaga, mumewe na Hellena (Mama Zarau)
"Kikanuni mgeni anapokutembelea hapaswi kuishia nje"

Ndivyo tulivyoelekezwa hapa, na hatukuwa na ubishi. Lazima kuingia ndani ili tuweze kuendelea kusonga mbele na safari yetu ya leo.