Sunday, March 4, 2018

KUZALIWA MARA YA PILI


 Jumamosi,
Shule ya Sekondari Kitungwa,
Amina Billy Msalya
Anapata Ubatizo katika Kanisa la Waadiventista Wasabato Kitungwa.

“Basi kulikuwa na mtu mmoja kati ya Mafarisayo, aliyeitwa Nikodemo, mtawala wa Wayahudi. Huyo alimjia wakati wa usiku na kumwambia: ‘Rabi, tunajua kwamba wewe ukiwa mwalimu umekuja kutoka kwa Mungu; kwa maana hakuna anayeweza kufanya ishara hizi ambazo unafanya isipokuwa Mungu awe pamoja naye.’ Yesu akajibu akamwambia: ‘Kwa kweli kabisa ninakuambia, Mtu asipozaliwa tena, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.’ Nikodemo akamwambia: ‘Mtu anawezaje kuzaliwa akiwa mzee? Je, anaweza kuingia katika tumbo la uzazi la mama yake mara ya pili na kuzaliwa?’ Yesu akajibu: ‘Kwa kweli kabisa ninakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Kile ambacho kimezaliwa kwa mwili ni mwili, na kile ambacho kimezaliwa kwa roho ni roho. Usistaajabu kwa sababu nimekuambia, Ninyi lazima mzaliwe tena. Upepo huvuma mahali ambapo unataka, nawe unasikia mvumo wake, lakini hujui mahali ambapo huo unatoka wala mahali unapoenda. Ndivyo alivyo kila mtu ambaye amezaliwa kwa roho.’ Nikodemo akajibu, akamwambia: ‘Mambo haya yanaweza kutukia jinsi gani?’ Yesu akajibu, akamwambia: ‘Je, wewe ni mwalimu wa Israeli na bado hujui mambo haya? Kwa kweli kabisa ninakuambia, Yale tunayoyajua tunayasema na yale ambayo tumeyaona tunatoa ushahidi juu yake, lakini ninyi hampokei ushahidi ambao tunatoa. Ikiwa nimewaambia ninyi mambo ya duniani na bado hamwamini, mtaamini jinsi gani nikiwaambia mambo ya mbinguni?’” —Yohana 3:1-12.

No comments:

Post a Comment