Tuesday, February 27, 2018

KUSHIRIKI SABATO NYUMBANI


Nyumbani ni nyumbani,
Wakati wa likizo yangu nilipata Baraka za kushiriki Sabato Mbili katika kanisa la Nyumbani la Nakatuba.
Tulipata kubarikiwa sana kwa mafunzo mbalimbali, kujifunza Lesson pamoja, Nyimbo na Mahubiri.
Ni Kanisa hili Mzee CK Msalya alikuwa na ndoto ya kuliona likikamilika, lakini muda huenda haraka mno. Ukamilikaji wake ni Changamoto kubwa sana kwa washiriki wa hapa, 
Wazee wa Kanisa walielezea mpango wa kufanya Harambee baadae mwaka huu ili kuendeleza pale palipofikiwa,
Familia ya Msalya pamoja na wadau wa Blog wameombwa kuendelea kutowatupa mkono washiriki wa Nakatuba.
Chochote kidogo kitakachokuwa kikipatikana kikasaidie kunyanyua Juu Kanisa la Bwana Nakatuba. 

No comments:

Post a Comment