Monday, January 8, 2018

KWAHERI YA KUONANA

Wapendwa Minoo na Penina,

Leo ni siku muhimu kwenu, baada ya kumaliza masomo ya msingi sasa mnaelekea Kitungwa kuendelea na maisha ya shule ya aina nyingine, masomo ya sekondari.
Tunasononeka kuwa sasa hatutakuwa nanyi  nyumbani kila siku kila saa, hatuwezi kucheka na kufurahi pamoja tena, mtakuwa mbali nasi. lakini twafarijika kwamba mnapata fursa nyingine muhimu kwenu katika kuyafikia maarifa.
Kwa kuwa Shule pekee, twaamini mtajifunza mengi ikiwemo kujitegemea na kufanya maamuzi kwa ajili ya maisha yenu ya usoni.
Sisi familia tunawatakia kila la kheri na fanaka kwa hiyo miaka minne mutakayokuwa Kitungwa.
KWAHERI YA KUONANA.

Msalya - MyFamily
Jumapili 07 Jan 2018

2 comments:

  1. Kila la kheri Amina na Penina
    Tunawaombea kher

    ReplyDelete
  2. Goodluck ladies and may the Good Lord keep you forever!!

    ReplyDelete