Tuesday, November 14, 2017

UOGAJI KATIKA SAUNA

Wajua Sauna ni nini?
Sauna, kama Bafu la kuogea ni ustaarabu wa miaka mingi wa Watu wa Finland. Karibu kila nyumba nchini Finland in Sauna yake.
Hiki ni chumba maalumu ambacho hupashwa joto kwa Kuni, Mkaa, Umeme au Gesi kwa ajili ya kuweka Mvuke, Moshi au Joto kwenye Sauna.
Watu huingia humu kuoga mvuke, Mvuke huu husababisha mwogaji kutoa jasho. Na kwa kutoa jasho huamini mwili husafishika na kuimarika.
Sauna yaweza kutumiwa na mtu mmoja mmoja au watu wengi kwa pamoja, wa familia moja au ofisini
Kila nyumba, na kila Ofisi ina chumba cha Sauna
 Chumba cha Sauna, Turku University Science Park.

No comments:

Post a Comment