Tuesday, November 7, 2017

SIMULIZI YA RIZIKI

Riziki yetu ya kila siku hutoka kwa Mungu.
Simulizi kuhusu Riziki zasema kwamba Mwenyezi Mungu hutuma Malaika wake kila siku ili kuwafikishia Riziki zao Wanadamu wote.
Ili kupata Riziki yako ya siku yakupasa kuwepo pahala ulipopangiwa kupokelea Riziki yako ya siku hiyo kwa muda muafaka uliopangiwa pia.
Malaika wasipokukuta pahala ulipopangiwa katika muda huo, huirejesha Riziki hiyo kwa Mwenyezi Mungu.
Wengi wetu tumekuwa tunakosa Riziki kwa kutokuwepo pahala sahihi katika muda muafaka.
Ndiyo maana Binadamu, kila kukicha twakimbizana huku na kule. Yote hayo ni katika kubahatisha, Riziki yangu ya leo nitaipokelea wapi na wakati gani?

No comments:

Post a Comment