Saturday, May 13, 2017

UCHIMBAJI WA JIWE LA SUMU YA NYOKA




Jiwe la kuondoa sumu ya Nyoka,
Maarufu sana Mikoa ya Kati na Kanda ya Ziwa.
Umewahi kujiuliza, kama jiwe ni mojawapo ya madini ya asili, na madini huchimbwa ardhini, Je jiwe la kuondoa sumu ya nyoka linapatikana wapi?
Inaaminika ukiumwa na Mdudu mwenye sumu au Nyoka, ukichanjwa kidogo likawekwa hilo jiwe, Basi litanyonya sumu yote iliyomo kwenye damu na litadondoka lenyewe.
Baada ya hapo ni kuliweka kwenye maziwa au maji moto ili kuondoa sumu iliyonyonywa.
Kwa taarifa yako,
Jiwe hili hutengenezwa kutokana na mifupa ya wanyama.
Yaweza kuwa mfupa toka kichwa cha nyoka au mkia. Lakini pia mfupa wa paja wa Ng'ombe.
Mfupa uliochaguliwa hukatwa katika vipande vidogo vidogo na kuvilainisha vizuri kwa Msasa.
Vipande hivi hufungiwa kwenye "foil" na kupashwa kwenye moto wa mkaa kwa dakika kati ya 15 na 20.
Baada ya hapo ni tayari kwa matumizi.

Imeandaliwa: kutoka habari za mitandaoni


No comments:

Post a Comment