Wednesday, May 17, 2017

HADITHI YA KUSISIMUA YA MSICHANA WA KICHINA

QIAN HONGYAN
Akiwa na umri wa miaka 4, Qian hongyan alipata ajali mbaya. Wakati akivuka barabara aligongwa na lori katika mji wa nyumbani kwao wa Luliang, Mkoa wa Yunman kusini magharibi mwa China. Qian alipoteza miguu yote miwili.
Babu yake akitumia mpira wa Kikapu, uliokatwa kidogo juu na kumvisha. Na kwa msaada wa magongo mawili madogo akaweza kujongea na kucheza na watoto wenzie. Mpira huu ulimfanya kujulikana kama "Basketball Girl", Msichana wa mpira wa Kikapu.
Pamoja na masaibu yote hayo, Qian hakukata tamaa.
Alijifunza kuogelea, na leo Qian ni mwogeleaji Bingwa katika michezo ya watu wenye ulemavu na amewahi kujinyakulia hadi medali ya dhahabu katika michuano mbali mbali ya Walemavu.

Hivi karibuni Qian amefanikiwa kupata miguu ya bandia. Qain anaishi na wazazi wake, Baba na Mama na anao wadogo zake wawili.              

sources
Qin Xie - Mailonline
Cina Oggi - China Underground.com
Adam Taylor - Business insider















No comments:

Post a Comment