Tuesday, November 8, 2016

TANZIA: DEBORAH RAYFORD MAINGU

Deborah hatunae,
Deborah binti Rayford Maingu amefariki dunia baada ya gari aliyokuwa akisafiria na wanae wawili kupata ajali.
Ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Noah iliyokuwa inatoka Nzega kuelekea Tinde na Lori aina ya Scania lililokuwa linatoka Kahama kuelekea Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea majira ya mbili kasorobo usiku  Jumapili,November 06,2016 katika eneo la Nsalala kata ya Tinde mkoani Shinyanga.
Mazishi yanapangwa kufanyika baadae leo nyumbani kwa Mama yake mzazi, eneo la Usanda nje kidogo ya mji wa Shinyanga.

1 comment:

  1. Taarifa ya karibuni ni kwamba mtoto mmoja, ambae pia alipata majeraha amefariki dunia.

    ReplyDelete