Friday, August 12, 2016

LIJUE ZIWA NGOZI

Ziwa Ngozi liko takribani kilometa 38 kutoka Mbeya mjini, kwenye safu za milima ya Uporoto. Ni Mita 2620 toka usawa wa bahari. Ukubwa wake ni Kilometa za mraba zipatazo 3.75
Kuna simulizi nyingi za kale kuhusu ziwa Ngozi, lakini wanasayansi wanasisitiza kuwa ni matokeo ya Volkano.
Ziwa Ngozi halina mto unaoingiza wala kutoa maji. Kuna samaki katika ziwa hili japokuwa hakuna shughuli za uvuvi kutokana na ugumu wa kulifikia na pia nyenzo za uvuvi.
Ni mojawapo ya vivutio vya utalii nchini mwetu.

No comments:

Post a Comment