Monday, May 30, 2016

PENYE NIA PANA NJIA

Walimwambia hataweza,
Alitumia Tindo na Nyundo,
Miaka 22 baadae aliwadhihirishia anaweza.
 Dashrath Manjhi.1934 -2007
Ni simulizi ya kale ya kweli ya Dashrath Manjhi.
Dashrath Manjhi aliondoka kijijini kwao  Gehlaur katika wilaya Gaya Bihar ya kwenda kufanya kazi za kibarua katika migodi ya Dhanbad, baadae alirejea kijijini na kumwoa Bi Phalguni Devi.
Dashrath akifanya kazi zake mbali milimani na mkewe Bi Phalgun akimpelekea chakula cha mchana. Siku moja katika harakati za kumfikishia mumewe chakula Bi Phalgun alitereza na kuanguka. Aliumia vibaya. Ilikuwa kazi kubwa sana kumfikisha kwenye matibabu katika hospitali ya kijiji jirani cha Wazirganj. Pamoja na kwamba ilikuwa umbali wa kilometa 10 hivi upande wa pili wa mlima ilikuwa ni lazima kuzunguka mlima kwa umbali wa zaidi ya kilometa 40.
Hapo ndipo wazo la Dashrath la kuwa na barabara ya kuwaunganisha na majirani zao lilipoanzia, lakini wanakijiji wenzie walimwona kama mwendawazimu anaewazia jambo lisilowezekana. Waliamini haitawezekana.
zana alizotumia zikioneshwa na mwanae
Dashrath aliweka nia ya kujenga njia ya wazo lake.
Alichukua Nyundo na Tindo, na kwa mikono yake kwa miaka 22 (1960 - 1983) aliweza kutengeneza barabara iliyopunguza  umbali kutoka mzunguko wa Kilometa 55 hadi njia ya mkato ya kilometa 15.
Alijipangia muda wa kutenda kazi hii, akiamuka alfajiri kutenda kazi za shambani kwake, na baadae kutengeneza barabara hadi mawio.

Hatimae alifanikiwa.
Dashrath alifariki tarehe 17 Agosti 2007 kwa maradhi ya kansa ya kibofu katika hospitali ya All India Institute of Medical Sciences (AIIMS), New Dheli na kupewa mazishi ya kitaifa na serikali.
Dashrath Manjhi - "Mountain Man"

SOURCE:
Mitandao

No comments:

Post a Comment