Monday, April 11, 2016

WATOTO WA MTAANI

Ubungo Bus terminal, leo asubuhi
Watoto wa mtaani,
Mtaani ndio nyumbani kwao. 
Wametelekezwa au kufiwa na wazazi wao. 
Lakini pia familia zingine wanatembeza watoto wao mtaani ili waende kupata hela. 
Wengine wanashinda njiani kwa sababu ya hali ya umaskini wa familia zao.
Wanafanya  kazi ndogo ndogo au wanaibaiba. Wamezoea kupigana na kuombaomba kwa ajili ya chakula. Biashara ya madawa ya kulevya ni kawaida kwao.
Wanalala mtaani bila ya kulindwa na mara kwa mara wanafukuzwa na polisi. 
Watoto wa mtaani wengi wanakabiliana na adha zote za mtaani, njaa, jua, mvua baridi na maradhi mbalimbali,vitendo vya vurugu na mengine mengi.

No comments:

Post a Comment