Tuesday, March 15, 2016

KELVIN IN DAR

 Dunia kama kijiji, mambo mengi yamerahisishwa. Hatimae Kelvin safari yake imemfikisha kwa mara ya kwanza kabisa katika jiji la D'Salaam. Tofauti na enzi zile Kelvin ameweza kufuata maelekezo na kufika mwenyewe bila kupokelewa na wenyeji wake.
Inanikumbusha nami mwaka 1980 nilipoingia jijini kwa mara ya kwanza. Niliposhuka stesheni kwa mara ya kwanza, ile picha niliyokuwa nayo ya jiji ilibadilika kabisa. Ni simulizi ndefu, lakini mimi kwa mwenyeji wangu nilifika kesho yake asubuhi baada ya kuwa nimewasili Dar.
Hakika teknolojia ya mawasiliano imebadilisha mambo mengi.

No comments:

Post a Comment