Tuesday, February 16, 2016

UMEWEKA ALAMA ?



Nimekumbuka leo kisa cha watu  wawili waliokwenda pahala kupitia mwitu mkubwa, Mmoja mwerevu mwingine mpumbavu. Mwerevu wakati wa kwenda alidodosha vipande vidogo vidogo vya mawe njiani, wakati wa kurudi vipande hivyo vilimsaidia kutambua njia ya kurudia. Mpumbavu alinyofoa vipande vidogo vidogo vya mkate na kuvitupa njiani alimopita, Kunguru walividonoa na kuvila, na wakati wa kurudi hakukuwa na alama yoyote, akapotea mwituni.
Dar Es Salaam nayo inabadilika haraka, kama huna alama zako huko mjini ipo siku utapotea.

No comments:

Post a Comment