Tuesday, November 10, 2015

NI SIMANZI.......

Bi Grace, Mama wa watoto waliofariki.
 Mazikoni, Makaburi ya Kingolwira Morogoro.
 Hapa ndipo walipopumzishwa wapendwa wetu Christina, Musheri na David
Waombolezaji wakirejea toka mazikoni
Bw. Kenedy. Baba wa marehemu
Huyu ndiye aliyenusurika katika mkasa huu.
Marehemu Christina
                                                                Marehemu Musheri
                                                           Marehemu David Mafuru
Jumamosi ya tarehe 07 Novemba 2015 ikianza vyema asubuhi, lakini ikiiacha familia ya Bw Kennedy na Bi Grace ikiwa na machungu na majonzi ya kuondokewa na watoto wao watatu kwa ajali ya kuzama kwenye dimbwi la maji.
Asubuhi hiyo Grace na wanae hawakwenda kanisani kama ilivyo kawaida yao, badala yake Grace aliondoka nyumbani maeneo ya mashambani, Mikese Morogoro kwenda kumjulia hali wifi yake maeneo ya Kingolwira, Morogoro.
Bw Kennedy nae katika kuhakikisha maisha yanasonga, akakodi Bodaboda kwa ajili ya kupeleka mikungu yake ya ndizi eneo la Mikese Mizani kwa ajili ya kuuza.
Watoto baada ya kuachwa nyumbani peke yao, katika michezo yao iliwafikisha maeneo ya mabondeni kwenye majaruba ya mpunga. Hapa ndipo walipopatwa na wazo la kuingia majini kuogelea.
Watatu waliingia majini kuogelea, na huo ndio ulikuwa mwisho wao.
Mmoja mdogo hakuingia majini alibakia na mavazi ya ndugu zake, na huo ndio ulikuwa uzima wake.
Mtoto huyu alikutwa na wapita njia, na katika kumhoji kutaka kujua kulikoni ndipo ikaja kudhihirika kuwa ndugu zake wengine watatu walikuwa wamezama majini, wamefariki dunia.
Hii ilikuwa mida ya asubuhi kwenye saa nne.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment