Wednesday, October 7, 2015

"JISIKU NI KABHAJO!"

Uncle (Late) Maingu Magoti with his wife Nyamaindi in 1974

Hakika muda ni fumbo la maisha.........
Muda huja na kupita, muda hauna mwanzo, muda hauna mwisho japo binadamu wameweza kuupima katika Sekunde, Dakika, Masaa, Wiki, Miezi na Miaka.
Imekuwa ni kawaida tu kusema wakati uliopita, uliopo na ujao. Siku ikipita imepita, jana imepita, leo ni leo na kesho haijafika.
Hata viumbe na mimea yote huendana na majira ya muda. Huzaliwa, hukua na hatimae hufariki. Hupita.
Kuna wakati kwa kila kitu, na majira ya misimu huja kulingana ma wakati, na hata uumbaji umeendana na wakati. Haiwezekani kupanda na kuvuna mpunga ndani ya mwezi mmoja na vivyo hivyo haiwezekani kwa Binadamu kuzaliwa na kuzeeka ndani ya mwaka mmoja, kila kitu kwa muda maalumu.
Muda unasemwa kuwa ni nguvu ya bure, muda hauna subira. Muda uliopita kamwe hauwezi kupatikana tena, kila wakati muda unaruka ukipita..........

No comments:

Post a Comment