Thursday, October 29, 2015

DAWA YA MOTO NI MOTO!!!

Ilikuwa ni sinema ya aina yake leo asubuhi, kituo cha njiapanda ya segerea.
Dereva wa Daladala lifanyalo safari za Gongo la Mboto Tandika T257 ADV, alimchomekea mwenzie Daladala lifanyalo safari za Gongo la Mboto Mawasiliano na kuvunja Side Mirror ya kushoto, likasepa.
Kufika njia panda akamkuta bado anapakia, kwa kulipa kisasi akashuka akaenda akavunja Side mirror ya Gari hilo la Tandika.
Madereva wote wakiwa wameshuka wakapimana ubavu, Bahati nzuri Dereva wa Mawasiliano alipata support ya abiria wake katika kumshushia kichapo dereva wa Tandika.
Pichani kifua wazi ni Dereva wa Tandika ambae shati lake liliraruriwa katika tafrani hiyo.
Tafadhalini tutumie barabara kwa uangalifu.

No comments:

Post a Comment