Wednesday, August 19, 2015

EXPEDITION TO THE GREAT WALL OF NYACHIRIGA (2)

 Safari yetu inapaswa kufika pale..........
 Ni lazima kuvuka vilima na mambonde vyenye mtandao wa mawe mengi
Bw. Beka Lazaro Ng’oko (kushoto)


“OBHUTINGO BHWA NYACHIRIGA” Ikimaanisha “Ukuta wa Nyachiriga” ni mojawapo ya historia ya kipekee isiyojulikana sana, na inayokaribia kufutika.
Ijumaa ya terehe 07 August 2015, kwa ushawishi  wa Nyachiriga Bright K. Msalya ninapata bahati ya kuutembelea ukuta huu wa kihistoria kama mojawapo ya kujifunza na kupata maelezo kuhusiana na Ukuta  wa Nyachiriga.
Safari yetu kutoka nyumbani kwetu Nakatuba umbali wa kilometa 23 hivi, (30 km kutokea Kibara Centre) kuelekea kaskazini magharibi ikatupitisha katika vijiji vya Bhulendabhufwe/Mkoko, Mwigundu, Bhuguma na hatimae Muchigondo na kisiwani Kubhwenyi. Kubhwenyi ni kisiwa kidogo kinachotenganishwa na kijiji cha Muchigondo na mfereji wa maji (mto mdogo) unaounganisha maji ya ziwa upande wa Magharibi na upande wa Mashariki.
Mwenyeji wetu wa kwanza Muchigondo anakuwa Bw. Beka Lazaro Ng’oko tuliyesimama kumwomba maelekezo ya njia ya kuufikia Ukuta wa Nyachiriga. Beka mwenyeji wa Muchigondo na Bhuguma anatuthibitishia uwepo wa “Obhutingo bhwa Nyachiriga”, na anatusindikiza kwa umbali kidogo na kutuelekeza ramani namna ya kuufikia. Kuufikia Ukuta wa Nyachiriga ni lazima kuvivuka vilima vitatu na mabonde yenye mtandao wa mawe mengi.

Itaendelea.......................

No comments:

Post a Comment