Tuesday, October 28, 2014

DUNIA KUWA GIZANI

WORLDWIDE - NASA has confirmed that the Earth will experience 6 days of almost complete darkness and will happen from the dates Tuesday the 16 – Monday the 22 in December. The world will remain, during these three days, without sunlight due to a solar storm, which will cause dust and space debris to become plentiful and thus, block 90% sunlight.
This is the head of NASA Charles Bolden who made the announcement and asked everyone to remain calm. This will be the product of a solar storm, the largest in the last 250 years for a period of 216 hours total. Reporters interviewed a few people to hear what they had to say about the situation with Michael Hearns responding “We gonna be purgin my n*gga, six days of darkness means six days of turnin up fam”.
Despite the six days of darkness soon to come, officials say that the earth will not experience any major problems, since six days of darkness is nowhere near enough to cause major damage to anything. “We will solely rely on artificial light for the six days, which is not a problem at all”, says NASA scientist Earl Godoy. Visit our website daily for more shocking news!

SOURCE:
HUZLERS.COM

ITS OVER



HISTORIA FUPI YA
CRAWFORD KURWIJIRA MSALYA. “CK”
04 Januari 1931 – 26 September 2014

Kurwijira Crawford Msalya alizaliwa tarehe 04 Januari 1931, Kijijini Nyambubhi, Kisorya  Bunda wakati huo ikiitwa wilaya ya South Mara. Baba yake akiitwa Msalya Maseme “Sekaseka” na Mama Bhituro Msema.
Mwaka 1937 Mzee Msalya alihama na familia yake kutoka Nyambubhi kwenda Nakatuba, Mwibhara.
Tokea mwaka huo hapa ndio pamekuwa makazi yake Bw Kurwijira Crawford Msalya.

FAMILIA.
Marehemu Kurwijira alimwoa Bi. Nyabhutwema Penina Magoti tarehe 17 Novemba 1951, ambae walijaaliwa kupata watoto kumi na mbili,  watoto walio hai leo ni watoto kumi.
Belly
Bright
Billy
Beria
Baruku
Bithia
Bora
Bahati
Bilshani na
Baasha
Marehemu Kurwijira amebahatika kupata wajukuu 34, lakini hadi anafariki ameacha wajukuu 30 walio hai.
Marehemu pia amebahatika kupata vitukuu wanane.
Peter CK
Penina
Belly
Pricilla
Billy
Miriam
Poulsen
BenGeorge.
Marehemu amefariki akiwaacha wadogo zake watatu kwa kuzaliwa.
Mwayai
Chausiku
Tabhu
IMANI
Mzee Kurwijira alibatizwa mwaka1989 na Mchungaji Makoko katika kanisa la Waadivenista Wasabato Nakatuba, na amekuwa mshiriki hapo hadi mauti inamkuta.

ELIMU NA UTUMISHI
Marehemu alipata elimu ya msingi kati ya mwaka 1944 hadi 1950 katika shule mbalimbali za Kitengule SDA (Paul School), Bunere SDA, Elusori, Bwasi na Nyambitilwa (Ushashi).
Utumishi wake ulikuwa katika Nyanja tofauti tofauti.
·         1952 – 55, Karani South Mara Native Authority
·         1955 -  57, Karani wa Mahakama, Ushashi – Utemi wa Chifu Masanja.
·         1957 – 61, Karani Namalebe Growers Cooperative Society
·         1975, Afisa Ulinzi MICO
·         1975 – 84, Bwana Shamba Mamlaka ya Pamba Tanzania, Mara

SIASA NA JAMII
Marehemu Mzee CK ametumikia pia nyadhifa mbalimbali za kisiasa na kijamii.
·         1955, alijiunga na chama cha TANU
·         1958, Kuingia TANU Youth League
·         1977, Kujiunga na CCM
·         1965 – 67, Diwani South Mara District Council
·         1968 – 75, Mwenyekiti wa Kijiji Nakatuba/Kata
·         2000 – 04, Mwenyekiti TASAF Nakatuba
·         1997 – 2005, Mwenyekiti CCM Kata ya Kibara
Pia Mzee CK kwa nyakati mbalimbali aliwahi kutumikia nyadhifa nyingine kati ya miaka ya 1958 na 1970, ambazo ni pamoja na:
o   Mjumbe Kamati ya Tawi la TANU Kibara
o   Mjumbe, Kamati ya fedha na DDC ya Baraza la madiwani
o   Katibu na mjumbe, Umoja wa Vijana Tawi la Kibara
o   Mjumbe wa nyumba kumi
o   Mjumbe wa Kanda, Chama cha Ushirika Nyanza
o   Mjumbe wa Tanu Wilaya na Mkoa
o   Mwenyekiti wa TANU Kata ya Kibara
o   Mzee Mshauri, Mahakama ya Mwanzo Nansimo
o   Karani Baraza la Usuluhishi, Kata ya Kibara
o   Mwenyekiti Shule ya Msingi Kitengule
o   Mwenyekiti shule ya Msingi Namalebe
o   Mwenyekiti Chama cha Ushirika cha Msingi, Nakatuba
o   Mjumbe, Chama kikuu cha Ushirika Mara, Mara Coop
o   Mwenyekiti Baraza la Kimila Nakatuba
o   Mjumbe wa CCM, Mkutano mkuu wa Wilaya na Mkoa

MARADHI NA MAUTI
Maradhi ya Mzee CK yalianza kujitokeza Desemba 2013, wakati huo akiwa ametembelewa na wanae na wajukuu nyumbani Nakatuba aliwasimulia tatizo alilo nalo la maumivu wakati wa kumeza chakula.
Kati ya mwezi Desemba 2013 na Januari 2014 alipata matibabu ya awali katika hospitali ya Mkombozi iliyopo mjini Bunda.
Mnamo April 2014, Mzee CK alianza safari ya kuelekea Dar Es Salaam kwa ajili ya matibabu akipitia Bunda, Mwanza,  Dodoma na Morogoro. Akiwa Morogoro alipata vipimo na uchunguzi katika Hospitali ya mkoa ya Morogoro. Hakuna tatizo lolote lililogunduliwa.
Mzee CK aliendelea na na vipimo vya uchunguzi katika Hospitali za Madona na baadae Tabata General Hospital ambao waligundua kuwepo kwa kwa tatizo la uvimbe kooni. Tatizo ambalo lilithibitishwa tena katika Hospitali za Hindu Mandal na Besta Diagnosis Kinondoni na ikashauriwa na Madaktari afanyiwe upasuaji.
Alilazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe tarehe 27 April 2014, ulioongozwa na Dr Mavura akisaidiana na Dr Katembo. Ilipendekezwa baada ya muda afanyiwe upasuaji wa pili kwa ajili ya kurejesha mfumo wa kawaida wa chakula.
Tarehe 27 May 2014 alilazwa tena Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na akafanyiwa upasuaji wa pili tarehe 30 May 2014, Upasuaji ambao haukufanikiwa na ikapendekezwa aendelee kubakia kwenye uangalizi wa madaktari wa mara kwa mara kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa tatu. Bahati mbaya wakati akiendelea kusubiria upasuaji huo afya yake ilikuwa ikiendelea kuzorota siku hadi siku. Pamoja na jitihada za uangalizi na uimarishaji wa hali yake, haikusaidia. Kuanzia tarehe 20 Septemba 2014 hali ilianza kudhoofu kwa kasi hadi mauti ilipomkuta tarehe 26 Septemba 2014, Saa moja na dakika tano jioni nyumbani kwa Mjukuu wake Bw Eddyson Msalya. Mzee CK alikata roho mbele ya familia yake, Mkewe Bi Penina, Mdogo wake Bw Mwayai na wanae Billy, Bilshani, Sarah na Beria.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
AMINA

WHAT A PAIN!

Ecclesiastes 3:1-14

For everything there is a season, and a time for every matter under heaven: a time to be born, and a time to die; a time to plant, and a time to pluck up what is planted; a time to kill, and a time to heal; a time to break down, and a time to build up; a time to weep, and a time to laugh; a time to mourn, and a time to dance; a time to cast away stones, and a time to gather stones together; a time to embrace, and a time to refrain from embracing;  

Friday, October 24, 2014

MUSOMI MASOTA: Kwaheri CK

Mzee Musomi Masota,
rafiki mkubwa wa Mzee CK, na hata wakati akiugua Dar Es Salaam ilikuwa haipiti wiki bila kumjulia hali.
Lakini Mzee Musomi hakuja kumzika rafiki yake, alikuja siku chache baadae..............
nikijiuliza kulikoni, lakini kumbe alikuwa sahihi kwani kama angekuwepo siku ya mazishi huenda  tusingekuwa nae pia.
Siku aliyokuja kutupa pole, baada ya kuona Kaburi la rafiki yake Mzee CK, uthibitisho kuwa rafikie hayupo tena, Mzee Musomi alizimia ikatulazimu sisi tena kumpa huduma ya kwanza.
Pole sana Mzee Musomi, kwani maisha ni lazima yaendelee............

Wednesday, October 22, 2014

SUPER RIDER

Riding to satisfaction
Karukekere

KUSUBIRIA MLIO WA PARAPANDA

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari za hao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na paraparanda ya Mungu, nao waliokufa katika kristo watafufuliwa kwanza; Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele’. (1Wathesalonike 4:13-17) - See more at: http://jicheki.com/bwana-yesu-yuaja/#sthash.GQxGNWNo.dpuf 
 
(1Wathesalonike 4:13-17)
Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari za hao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na paraparanda ya Mungu, nao waliokufa katika kristo watafufuliwa kwanza; Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele’. (1Wathesalonike 4:13-17) - See more at: http://jicheki.com/bwana-yesu-yuaja/#sthash.GQxGNWNo.dpuf

URITHI

Kwa kweli, urithi una thamani fulani, lakini hekima ina thamani kuu kuliko vitu vya kimwili.

KAMONGO

Kamongo,
baada ya kuadimika muda mrefu sasa wanapatikana tena, shukurani wadau wa uhifadhi wa mazalia ya samaki ziwani.
Kuna simulizi kuwa wanawake walikatazwa kumla kutokana na utamu wake uliotukuka.
Na sasa anazua changamoto miongoni mwa waumini kuwa ni halali au si halali kuliwa,
Sababu kuu ikiwa ni kwamba hana mapezi,
Najiuliza, ni kweli Kamongo hana mapezi!

ONCE UPON A TIME

Those old good days are gone,
Tunaililia Nakatuba yetu,
Nakatuba ile yenye rutuba tele
Miti ya kila aina
Nakatuba ya asali na maziwa,
Haipo tena leo, imegeuka jangwa........
Ni milima ya mawe tu sasa.