Monday, March 18, 2013

CHINYAMBWIGA HII



March 16th, 2013 by Stella Mwaikusa
Shule ya msingi ya Kinyambwiga iliyopo kata ya Guta wilayani Bunda, inakabiliwa na uhaba wa madarasa na madawati hali inayowapa wakati mgumu walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi wanalazimika kusomea chini ya miti huku wakikalia mawe na wengine wakikalia mabanzi.
Mwalimu wa somo la stadi za kazi darasa la sita B Kastori Mng’ong’o, anasema inamwia vigumu kufundishia chini ya mti kwani watoto wanakosa utulivu na kuiita hali hiyo kwamba ni “msingi  mbaya kwa wanafunzi hao.”
Anasema wanafunzi wakiwa hapo nje wamekuwa wakipoteza utulivu pale wanapoona mtu au gari linapita,  na kuondoa usikivu ambao ni mhimu sana kwa mtoto katika kujifunza.
Mwanafunzi wa darasa la sita Ubwe Juma anasama inampa wakati mgumu kupangilia mwandiko wake, kwani mara nyingi mawe anayoandikia hutingishika na wakati mwingine kudondoka kabisa.
Anasema pamoja na mwandiko kuwa mbaya bado suala la usafi kwao ni gumu kwani mawe hayo yana vumbi na kujikuta wakisoma huku wakiwa wamechafuka.
Mwalimu mkuu wa shule ya Kinyambwiga Leornald Mukama anasema kumekuwa na mipango ya kujenga madarasa lakini bado wanasubiri kwani yeye hana uwezo wa kufanya lolote.

Source: Jamii Forums

No comments:

Post a Comment