Friday, November 2, 2012

NGUVU YA AJABU YA MISIBA

Kuna nguvu ya ajabu katika Misiba.
na ndiyo maana tunapaswa kumshukuru Mungu kwa yote.
Ndugu, jamaa na marafiki tuliopotezana miaka mingi au muda mrefu umepita bila kuonana, mara nyingi tumekutanishwa kwa nguvu ya namna hii.
Kushiriki misiba ya wapendwa wetu.
Malembo haupo nasi sasa, lakini ni wewe umetukutanisha tena wengi ambao tulikuwa hatujaonana miaka mingi.
Kando  Magolinya, wazee wetu wa Nakatuba sasa. ingawa anasema yuko Geita muda mrefu. Hatujakutana yapata miaka 35 sasa.
 Fred Simbua, miaka kadhaa sasa tokea msiba wa Hokororo kule Kigamboni, japo mjini humu humu.
 Rukia Nyajirali, Dada yangu toka Bwai, Bongo hapa hapa lakini miaka sasa tokea Harusi ya Bin Hussein kule Green Rombo miaka kadhaa hatujaonana.
 1996 akileta Barua ya Posa pale kwangu Ubungo, Mr Mkaruka kaka wa Malembo zaidi ya miaka kumi na tano ndio tunakutana tena. Sasa wengi walimwita Leni.
 Esrom Makoroma Bhinamo, kijana wa nyumbani huyu lakini karibuni zaidi ya mwaka ndiyo tunaonana tena
 Geofrey Etutu, Mchambwe. Nimeanza kumsikia takribani miaka kumi sasa, na msiba huu umetukutanisha ana kwa ana
 Binti Stefano Malekela, tumepata kukutana mara moja na sikumbuki ni lini, lakini hakika muda mrefu sasa
 Omwende Thoma Lisso, tunakutana kwa mara ya kwanza
DJ Maregesi, Mchambuzi na mtangazaji pale Redia Morning Star. Pamoja na kumsikia mara kwa mara akiunguruma Redioni, mara ya mwisho kukutana ni miaka zaidi ya mitano hivi.

No comments:

Post a Comment