Tuesday, July 10, 2012

UZALISHAJI UMEME TOKA KWENYE TAKA TAKA

Takataka ni kero mitaani ila zinaweza kubarika na kuwa mali ghafi nzuri sana ya kuzalishia gesi amambayo inaweza kutumika kupikia ama kuendeshea mitambo mabalimbali ukiwemo wa kuzalisha umeme. Gesi hii ijulikana kama prodyusa gesi (producer gas)  au kiswahili sahihi kinaweza kuwa gesi zalishi. Hapa wataalamu wa kishwahili watanisaidia (^_^). Gesi hii inaweza kuzalishwa kutoka kwenye taka taka za aina zote kwa kutumia teknolojia ya kutengeneza gei (gtasification). Teknolojia hii kwa kutumia joto, ina badili taka taka hizi kuwa muchanganyiko wa gesi za carbon monoxide, methane (biogas/ gesi mbolea) na hydrogen. Hili linawezekana kwa vile carbon iliyoko kwenye taka taka inachomwa chini ya kiwango chake cha kawaida na kutengeneza carbon monoxide badala ya carbon dioxide ambayo hupatikana pindi carbon ikichomwa asilimia mia. 

Takataka zozote zinaweza kutika. Takataka za mijini ama mashambani. Kwa takataka kubadilishwa kuwa gesi kwa kutumia teknolojia ya gasification, kuna kiwango maalumu cha unyevunyevu kinapaswa kizingatiwe (< 30%). kwa takataka zambazo zinakiwango cha juu cha unyevunyevu, teknolojia nyingine hutumika ambazo hutumia vimelea vya asili kutengeneza gesi badala ya kutumia joto.

Hatua za kuzalisha gesi kutokana na takataka.

1. Takataka zinachambuliwa ili kutenganisha zile zinazochomeka na zisizochomeka. Hili linawezekana kwa kutumia mitambo ya kutenganisha takataka hizi ama kusipela dampo na kuzichimbua baada ya miaka kadhaa. Hii itasaidia wadudu kula sehemu ya takataka inayolika na kuacha sile takataka zisizolika ambazo ndizo zinafaa kutumiwa katika gasification.
Kisha taka taka hizi zinachanwa chanwa vipande vidogo vidogo na kutengeneza matofali madogo madogo ambayo yanaweka kwenye mtambo na hatimaye kubadilishwa kuwa gesi. 

 
a) Taka taka zilizochimbwa toka dampo 




b) zinajazwa kwenye chekecheo kuondoa udongo kabla ya kuchanwa






    
c)
d)
e)
 

  
f) vitofali (briquettes)  vidogo vidogo vilivyotengezwa kutokana na taka taka

mitambo tofauti inatumika kutengeneza vipande vidogo zaidi ya hivi. Mfano kwenye picha inayofuata masalia ya kiwanda cha nazi (vifuu na nyuzi) yametumika kutengenezea hivi vipande vitakavyotumika kzalisha umeme na joto kuendeshea kiwanda hicho cha nazi.
aina hii hujulikana kama pellets 
nazi zikiingizwa kiwandani 
mabaki yakisubiria kufanywa  pellets 
mtambo wa kutengenza pellets
2. Hatua ya pili, gasification. 
  

  
Mtambo wa kutengeneza gesi (downdraft gasifier) 
   
     
   
gesi iliyotengenezwa ikiwaka ikiwaka 
3. Mbali na kupikia majumbani, gesi hii inaweza kutumika kuzalisha umeme kama mbadala wa gesi ya asili. Mitambo inayotumika ni kama vile gas turbine ama gas engine 


2 comments:

  1. Uncle we urgently need the Technology in Kinyerezi.
    May FOCONA take part??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Definitely YES, that is a right place for FOCONA.
      Let us plan, I believe we shall succeed.

      Delete