Thursday, May 17, 2012

NANI ALAUMIWE??

Nani alaumiwe???????
Hali ya mitaro ya maji barabara ya kwetu Kinyerezi.
Imejaa takataka na michanga na mingine imezibwa.
 Walaumiwe City kwa kutokufika kuisafisha kwa wakati?
 Alaumiwe Mkandarasi ambaye hakumwekea mwananchi sehemu yake ya kupitia
au
Alaumiwe mwananchi aliyeziba ili kupata nafasi ya kupita na gari yake?
 Alaumiwe aliyepunguza miti yake na kugeuza mtaro sehemu ya kutupia matawi hayo?
Au alaumiwe aliyegeuza mtaro kuwa jalala?
Hii ndiyo Road Drainage system ya kwetu Kinyerezi, Manisipaa ya Ilala, Dar Es Salaam

1 comment:

  1. wote ni wa kulaumiwa. kila mmoja kachangia kuharibu hali iliyopo.
    iwapo kila mtu akafanya sehemu yake kuboresha mazingira, hali itakuwa nzuri sana.

    ReplyDelete