Monday, March 5, 2012

KIKAO CHA 15 CHA CHENDANE

Jana ilikuwa ni siku ya kikao cha 15 cha CHENDANE FOUNDATION, kikao kilifanyika Kipunguni mwenyeji wetu safari hii ni Bw. Eddyson.

Wajumbe wakijua ni kikao cha UChaguzi wa viongozi walianza kuingia mapema, pengine kumalizia Kampeni ambazo zimekuwa zikiendelea kwa zaidi ya mwezi sasa.

Mjumbe asiyetambuliwa, "Jaluo" lakini mhudhuriaji mahiri alikuwepo pia, tena mapema.....

Jaluo, Malembo, Agness

Mama Chai, Silla

Kikao kikaanza na ajenda zake za kawaida, wajumbe wakajadili, wakawasilisha michango yao kama kawaida

Mama Chai, Beria, Eliud

Ufatiliaji na umakini wa hali ya juu

Hatimae ikawa wakati wa Viongozi wa Muda waliokuwa wakiongoza kupisha Kigoda kutoa nafasi ya uchaguzi mpya wa viongozi kulingana na Katiba kufanyika.

Mwenyekiti wa muda ikabidi atafute sehemu nyingine ya kupozi

Mwenyekiti wa Muda, Bw Eliud akachukua usukani na wajumbe wakajadili namna bora ya kuwapata viongozi

Baada ya majadiliano, kura zikapigwa
na baadae kuhesabiwa mbele ya mashahidi


Mwenyekiti msimamizi wa uchaguzi akatoa matokeo

wenye kushangilia walikuwepo baada ya kupita mchuano huo mgumu

Mwongozo wa Msimamizi katika utangazaji wa matokeo

Matokeo yakaonyesha ifuatavyo:
Mwenyekiti - Billy Msalya
Makamu Mwenyekiti - Eddyson Hamisi
Katibu - Sospiter Kwesi
Mweka Hazina - Eliud Kaitira
Mjumbe - Kulwa Malembo
Mjumbe - Jackson Kaigi


Mwenyekiti Mteule na Katibu wake

Katibu Mteule akikabidhiwa mikoba

Mwenyekiti akarudi ulingoni kukamilisha kikao.
Pita pita ya Kamera upande mwingine ikamufuma mdau Bj Jnr akiserebuka kushangilia matokeo ya uchaguzi wa kura zilizopigwa. lakini haikujulikana alikuwa upande upi wa wagombea.......
KIKAO KINACHOFUATA CHA KUMI NA SITA KITAFANYIKA TAREHE 29 APRIL 2012 NYUMBANI KWA Bw. ELIUD KAITIRA, ULONGONI GONGO LA MBOTO

1 comment: