Monday, January 9, 2012

DARISALAMA KWELI MJINI SHULE

Jioni moja wakati wa kutoka ofisini tunamkuta mheshimiwa huyu nje kwetu.
Haijulikani imekuwaje yuko chini namna hii? Kaanguka au namna gani hatujui.............
Wasamaria wema wakawepo kumsikiliza na kumsaidia.
Akasema anakaa mitaa ya Kawe, anatokea mitaa ya Machinga kumtafuta jamaa yake ampe hela ya dawa maana anaumwa. Kufika hapa kaishiwa nguvu kaanguka.
Wasamaria wema wanamuuliza kama amekula au la....

Anasema hajala, lakini shida yake kubwa yeye kwa kuwa anaumwa anaomba Shillingi elfu tatu tu ili akapime Malaria hospitali.
inakuwa mtihani kwa wasamaria...........................
Hata hivyo wasamaria wengine wanajitolea kumnunulia soda.
itamfaa labda kidogo kupata nguvu akisubiria kupata msaada wa shillingi 3,000/= za kupimia malaria

Kesho yake tunahadithiwa alipata mfadhili wa shillingi 5,000/=, na baada ya kuzipokea alipata nguvu za kurudisha chupa tupu ya soda pale ilipokuwa imenunuliwa na wasamaria wa mwanzo.

Makubwa haya.............

Kweli mjini shule.......

No comments:

Post a Comment