Wednesday, December 28, 2011
TANZIA - KURURETERA NYAKUJERWA
Kururetera Nyakujerwa Maande
Taarifa zilizoifikia blog yetu, Ndugu yetu amefariki jana majira ya alasiri huko nyumbani Kisorya.
Mipango ya Mazishi inaendelea Kisorya.
Ndugu wa Dar Es Salaam tunataraji kukutana baadae jioni kuangalia namna ya kushiriki na kuwakilishwa.
HIVI NDIVYO NILIVYOIPITISHA SIKUKUU YA X MAS
Mapema asubuhi, siku ya sikukuu, Minoo, mimi na Manyama tukitafakari itakuwaje siku hii
Tukalazimika kuzuka dukani kwa Mangi, walau kupata mchele ili kubadilisha mlo wa sikukuu
mdau Issaya
Baadae Blogger akaingia kijiweni/masikani kwa stori za kupitisha muda
Mdau wa maskani
Na baadae mapema tukajisalimisha home kwa ajili ya kuwahi matukio muhimu kwenye Luninga kwa siku hiyo ya sikukuu, huku wadau wengine wakirejelea homeworks zao
Mungu ni Mwema, sikukuu imepita salama salimini.
Tukalazimika kuzuka dukani kwa Mangi, walau kupata mchele ili kubadilisha mlo wa sikukuu
mdau Issaya
Baadae Blogger akaingia kijiweni/masikani kwa stori za kupitisha muda
Mdau wa maskani
Na baadae mapema tukajisalimisha home kwa ajili ya kuwahi matukio muhimu kwenye Luninga kwa siku hiyo ya sikukuu, huku wadau wengine wakirejelea homeworks zao
Mungu ni Mwema, sikukuu imepita salama salimini.
Tunaisubiria Christmas ingine ijayo Mungu wetu akitujaalia
Tuesday, December 27, 2011
KARIBU MDAU JANETH
WADAU WA IDARA YA USHIRIKA BAGAMOYO
Jumamosi,
tarehe 24 Desemba 2011 wakati maandalizi ya X Mas yakiendelea kwa walio wengi, na ahueni ya maafa ya mafuriko ikianza kurejea taratibu, mimi na Mdau Herman Joseph tukawa njiani kuelekea Bagamoyo. Kwanza kuangalia athari za mafuriko kwa Mama Mkwe wangu Amina Kazinyingi aka Binti K pale Bagamoyo na pia kutoa salamu za pole kwa familia ya Rafiki na Ndugu wa siku nyingi Bw Hassan Salum Mirambo.
Kukaribia daraja la Kawe, tukapambana na mnyororo wa pande zote mbili, lakini nafuu iliyopo ni kuwa sasa panapitika angalautarehe 24 Desemba 2011 wakati maandalizi ya X Mas yakiendelea kwa walio wengi, na ahueni ya maafa ya mafuriko ikianza kurejea taratibu, mimi na Mdau Herman Joseph tukawa njiani kuelekea Bagamoyo. Kwanza kuangalia athari za mafuriko kwa Mama Mkwe wangu Amina Kazinyingi aka Binti K pale Bagamoyo na pia kutoa salamu za pole kwa familia ya Rafiki na Ndugu wa siku nyingi Bw Hassan Salum Mirambo.
Nyumbani kwa Binti K, athari za mafuriko zikiwa zimeicha nyumba hoi taabani japo maji yaliyoizingira sasa yakiwa yameondoka
Shukurani kwa mifereji ya dharura iliyotengenezwa kuondoa maji na kuyaongoza kwenye mfumo wake wa kawaida
Tukapata nafasi ya kufika kwa Mdau wa Idara ya Ushirika Bagamoyo, Bw Sango ili tuweze kufika pamoja kwa familia ya Bw Hassan Salum
Baadae tulielekea kwa familia ya Hassan ambapo tulikaa nao kwa muda kiasi
(Kanuni za kimaadili zikanifanya nisichukue picha zozote pale chumba cha eda) Baadae tukapata nafasi ya kubadilishana mawili matatu pale Alpha Motel, palipoasisiwa na Marehemu George
Patrick Chomola na Herman Joseph
Juma Mwanambara in Blue kanzu
Shemeji Mubaraka, kulia
Hakika ni jambo la kushukuru Mungu kwamba sisi bado ametupa uhai.Kwa sababu katika dodosa dodosa zetu nilikuta kwamba tokea October 1982 nilivyoripoti kwa mara ya kwanza Idara ya Ushirika Bagamoyo, wenzetu wengi tuliowakuta wakatupokea au waliokuja baadae hawako nasi tena.
Mwenyezi Mungu uwapumzishe kwa amani wote waliotutangulia
- Mzee Mkodo
- Mujos
- Bruno
- James Wamalwa
- Mwakalinga
- Modibwa
- Godfrey Hassan
- Joseph Kabelwa
- Fatuma
- Hassani Salum
MUNGU UWAPUMZISHE PEMA PEPONI AMINA