Tuesday, December 20, 2011

MVUA KUBWA DAR

Dar pamoja na vitongoji vya jirani leo usiku kumekuwa na mvua nyingi iliyoandamana na radi.
Kama kawaida ya mji wetu usiopangiliwa, mafuriko yameripotiwa sehemu mbali za jiji.
Binafsi nimeshuhudia mto msimbazi, Daraja la Kinyerezi ukiwa na maji mengi kwa mara ya kwanza mwaka huu. Nimepitia Mbozi Road nikakumbana na mafuriko makubwa pale karibu na Konyagi
Mabibo Relini palifurika pia leo, Kwa Mtogole ndiyo usiseme, daraja hakuna tena.
Picha za Mabibo Relini zilizochukuliwa na mdau wa Blog mapema asubuhi wakati mvua nyingi zikiendelea zikionesha magari yaliyokuwa yamesukumwa na maji pembeni kabisa

1 comment: