Monday, November 14, 2011

WATU BILION SABA DUNIANI - MAMBO SABA YA KUSTAAJABISHA

Kutoka www.cbsnews.com
Dunia imefikia hatua kubwa: Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa idadi ya watu duniani walivuka bilioni saba ilipotimu usiku wa manane wa tarehe 31 Oktoba 2011.
Kwa bahati mbaya, bilioni saba si sababu ya msingi ya kusheherekea, kwani ongezeko la zaidi la watu laweza kuleta matatizo zaidi.

Ulimwengu haujawahi kuwa na watu wengi zaidi. Tunaongezeka milioni 80 kila mwaka, sawa na idadi ya watu Ujerumani. Lakini kiwango cha ukuaji kwa dunia yetu kinaporomoka.Mwaka 1950 wastani wa watoto kwa kila mwanamke ilikuwa watano, Lakini leo ni watoto 2.5 kwa kila mwanamke.

Katika baadhi ya nchi, kiwango cha chini ya kuzaliwa ni tatizo. Nchini Italia, kwa mfano, wastani wa watoto kwa kila mwanamke ni 1.2, chini ya kiwango, hii ina maana miaka ijayo wazee watakuwa wengi kuliko vijana.

Watu Bilioni saba siyo tatizo kuhusiana na nafasi, Kama kila mtu katika ulimwengu wangesimama bega kwa bega, tungeweza kuenea ndani ya mipaka ya jiji la Los Angeles.

Hakuna mtu duniani anaepaswa kufa kwa njaa.Kwa mfano mwaka jana dunia ilizalisha chakula tani bilioni 2.3 za nafaka za kutosha kulisha watu bilioni 9 hadi 11. Hata hivyo, tatizo ni kuwa asilimia 46 tu ya kiasi huenda vinywani mwa binadamu na kinachobakia hulishwa wanyama hasa wale waliwao na hivyo kusababisha watu bilioni moja kushinda na njaa kila siku.
Kama idadi ya vegans ingeongezeka, basi dunia ingejitosheleza kwa chakula.

Mzigo mkubwa kwa rasilimali duniani.Si sana kuhusu idadi ya watu, kama ni idadi ya kaya. Kama ilivyo kwa Watu sita wa kaya moja kutumia jokofu moja hutumia nishati pungufu kwa kila mmoja ukilinganisha na watu sita kila mmoja akitumia jokofu lake.

Elimu ni kigezo kikubwa katika kudhibiti ongezeko la watu.
Vijana wanapokuwa shule muda mrefu, huchelewa kuoa/kuolewa na hivyo kuchelewa kuanza
kupata watoto. Na pia wanapoelimika hupendelea kupata idadi ndogo ya watoto.

Katika dakika tatu tu, watu 900 wanazaliwa, watu 360 wanakufa, na dunia inakuwa na ongezeko la watu 540.

No comments:

Post a Comment