Friday, November 11, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - VYOO VYA KWETU

Vacation yangu imeendana endana na simulizi za miaka hamsini (50) ya uhuru.

Tafakari yangu ikanipelekea kukumbuka matumizi ya vyoo, kwa wenzetu walioendelea choo ni muhimu sana kama sehemu ya nyumba bora.

Na kwa teknolojia hii ilivyo sasa, nyumba nyingine ukipata kuingia chooni utashangaa.
Hutachoka kuwemo chooni.

Ukarabati wa choo ukiendelea.
Nilipokuwa Nakatuba vacation safari hii, ukiona defostration ilivyo sasa nikakumbukia enzi zile za vyoo vya wazi. Popote unaacha mzigo na ni kwa sababu misitu na miti mingi ilituficha. Sasa hivi thubutu, kila sehemu iko wazi. wakati ule vyoo vyenyewe vya kuhesabu. Pale kwa fulani....., au kanisani, au Shuleni, au kule Stoo na sehemu namna hiyo.............

Lakini Loh, sidhani kama kuna mabadiliko ya kujivunia baada ya miaka 50 ya uhuru.
Nikaelekeza Kamera yangu sehemu nilizopitia, Na kwa jinsi nilivyojionea njia yote Nyanguge - Bunda - Kibara, wote hupendelea kuweka vyoo vyao mbele ya nyumba (Upande wa Barabarani)
Njiani ikawa si rahisi kupata taswira, hivyo nikajielekeza zaidi nilipokuwa safari za ndani.

Shule ya msingi Namalebe

Choo cha shule, hiki ni cha shimo matundu manne kwa wanafunzi wavulana na wasichana zaidi ya mia nne pamoja na walimu wao.

Kimejengwa takribani pahala pale pale palikokuwa na choo tulichokitumia hapa shule miaka 40 iliyopita, na mabadiliko ninayoyaona ni kuwa hiki cha leo kimeezekwa bati na cha kwetu kilikuwa open.

Hiki nilikiona kule mabhui merafuru

Hiki kina provision ya kufanya usafi kwa kutumia maji, na kina mlango lakini unaofunguka hata kwa upepo

Nilikuta net za mbu za msaada zikiwa zimetumika kwenye choo hiki huko Karukekere

Kibara mjini, maeneo ya Stand

Bar moja mjini Kibara, na hiki ni maalumu kwa wateja aina zote

Nakatuba

Choo na Bafu Nakatuba,
watu wengi tofauti na zamani sasa wanaogea mabafuni majumbani kwao na si mabafu ya wazi visimani

Kiwangwa, wilayani Bagamoyo

1 comment:

  1. Duh! inahuzunisha sana, ukizingatia wengine tumesomea mambo hayo.

    inabidi kifanyike kitu tena kwa haraka kubaadili hali hii.

    Muungu atujalie.

    ReplyDelete