Friday, November 4, 2011

ADHA YA MAFURIKO


Kingo kuziuia maji ni muhimu. ukifanikiwa kuweka kabla ya maji kukufikia ni vyema, la hasha jitahidi kuzuia hata kama yameshafika.


hatimae utafurahia matunda ya kazi yako. baadaye ni kazi ya kutoa maji yalioingia ndani. utatumia pump kama ni mengi au kupiga deki.


juhidi sisiishie getini pekee, unazuia hadi ndani vyumbani. lengo ni kuokoa vitu vyingi kadri uwezavyo. ni wazi kuwa hutookoa vyote!

maji yakishamiri, unahamia gholofa za juu ili kujiokoa. kwa waishio magholofani, wana haueni. hata kambi za uokoaji zipo magholofani



kina cha maji kinavyoongezeka, njia pekee ya usafiri ni magari makubwa au boti. magari madogo hayafui dafu ndani ya maji mengi.



jitihada zote zinalenga kufanya maji yatumie barabara kuelekea baharini. hivyo barabara zinageuka mito. kwa bahati nzuri, barabara karibu zote mjini ni za rami au zege.


mitaa yote ni mito, au mabwawa iwapo maji yamekwama.


kila mtu anajitahidi kuondoa maji kwake na kuyaelekeza kwingine. unaweka uzio, kisha unapump maji yatoke


inaposhindikana pa kuelekeza maji kwa haraka, basi maji yanaoza na harufu mbaya ya uvundo inashamiri.

maji ya mafuriko yanachanganyika na maji taka. unaweza kuvuta taswila hali inakuwaje.


basi ukishindwa kuendelea kuvumilia harufu, au ukiishiwa hifadhi ya chakula, basi inabidi uhame kuelekea kwenye kambi zilizo andaliwa au kwa jamaa walio maeneo yasiyoathirika au unakodi vyumba kwenye maghorofa.


malori ndio usafiri muafaka kwa masafa marefu.


hata wanyama pia wanatafuta pa kujihifadhi, japokuwa makazi yao ni majini.






1 comment:

  1. Thanks for the information and post.
    Hopefully wadau wengine nao wataanza kutujuvya from where they are.
    what they need to do is just accept my invitation sent to them earlier.

    ReplyDelete