Friday, June 3, 2011

SIKU KINYEREZI ILIPOPATA MAAFA 21.05.2011

Gari lilivyo baada ya ajali

Tarehe 21.05.2011



Bila kutarajia ikaja kuwa siku itakayobakia kwenye kumbukumbu za wana Kinyerezi kwa muda mrefu.


Siku hiyo majira ya mchana, Gari ya jirani yangu Miraji Abdallah "Mwamba" ikiendeshwa na mwanae Salum. akitokea kuchota maji Majumba sita akiwa kabeba pia vijana wenzie waliokuwa wakitokea mpirani ilipata ajali na kusababisha vifo vya vijana wanane papo hapo na majeruhi wengi.


eneo lenyewe ni kati ya Daraja la Kinyerezi na Pub ya kilimani, maarafu Njia panda ya Zowo Camphali ilikuwa ya kutisha eneo lenyewe la ajaliKishimo hiki, kilichokuwa chanzo cha ajali katika kukikwepa...Kesho yake 22.05.2011 nikapata nafasi ya kushiriki mazishi ya vijana wanne kati ya wanane waliofariki, hali ilikuwa ya majonzi makubwa, na watu wengi wa rika mbali mbali wa Kinyerezi walihudhuria mazishi hayo.


vijana ndiyo kwanza wakichipua na matumaini mapya, lakini nyota zikazima ghafla




Sheikh wetu mkuu alikuwepo kuwafariji wafiwaMwenyekiti wa mtaa Mheshimiwa KafunyaMheshimiwa bankoleWazee wetu, NurdinWanaharakati, Nyangaliro "Osama" Hakika ilikuwa siku ya majonzi makubwa..........


ambayo itachukua muda kusahulika miongoni mwa Wana kinyerezi








Bwana alitoa.............................


Bwana ametwaa..........................


Jina lake lihimidiwe.


Walale pema vijana wetu.

No comments:

Post a Comment