Monday, May 16, 2011

WADAU WAJITOKEZA KIKAO CHA SITA CHA WANANDUGU

Mwenyekiti wa Kikao cha Wanandugu, nilikuwa nimelala Bagamoyo kwa ajili ya kukamilisha shughuli za kikazi, na baadae kuwahi kikao cha wanandugu kule Mbagala.

Kikao cha sita kilipangwa kiwe tarehe 01 Mei 2011Wadau wakaitikia mwito na kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kikao hichi huku kwetu Uswazi
njia za kwetu huku si mchezo

sehemu nyingine lazima kusubiriana

na lazima kuwa na wataalamu wa kusoma ramani waliobobea

Naam, huku ndiyo kwetu Mbagala, hapa nyumba pale jalala

Lakini hatimae wageni waliwasili, na kupokewa na wenyeji wao Bw Titus Gunze kwa bashasha na furaha tele

Na baadae kikao kiliendelea kama kawaida




ajenda nyingine zilihitaji kukuna vichwa na busara ya hali ya juu

huku wajumbe wakichambua huku na kule






Lakini hatimae kikao kilimalizika, na wajumbe wakarejea makwao salama salimini.Kikao chetu kifuatacho kitakuwa Kitunda tarehe 29 Mei 2011 na Mwenyeji wetu safari hii ni familia ya Bw. Kulwa Malembo.


Tutaonana huko

No comments:

Post a Comment