Monday, March 28, 2011

BAGAMOYO VEKESHENI

Jana jumapili, nikawa nimetakiwa kwenda Mjini Bagamoyo kikazi.

Ikabidi kumuunganisha na Mzee CK, yeye aliplani kwenda kumusalimia mchambwe Mr Hadji.

Manyori na CK nao wakadandia trip.

Blogger kama kawaida akaweka pembeni Olympus na Kinokia

Njiani CK Jr akawa akivutiwa na taswira mbali mbali na kuweka kumbukumbu..... Mojawapo ya Taswira, ni Total Mlimani City. Kazi moja safi sana ya kampuni yetu ya Delmonte Breki ya kwanza ikawa maeneo ya Soko jipya kwa ajili ya breki fasti Nikapata bahati ya kukutana na Bwana Kitwana, jirani yangu miaka ile ya late 1980 na early 1990 na baadae office mate pale BADECO BEACH HOTEL
Breki fasti kila mtu kwa chaguo lake

chai ya mkandaa na chapati..
Supu ya kolekole................
Supu ya mbuzi...................
Tukapata nafasi ya kupatembelea hapa, Nyumba niliyoanzia maisha ya kupanga Bagamoyo Oktoba 1982. jirani na kwa Mzee Sudi, maarufu sana Bagamoyo enzi hizo akimiliki mabasi kadhaa ya abiria Dar - Bagamoyo
Tukapitia Customs ya miaka hiyo kuangalia bahari..........
na baadae kuelekea Makumbusho kule misheni, maarufu kama mantep

Pametulia...
Wadau wakashangaa shangaa humo ndani baada ya kuwa tumelipia buku na nusu kwa kichwa ili kupata ruksa ya kuingia kushangaa............

a nice place to visit
Kasiki, made in Austria in 1870
Mbuyu uliotumiwa na Nurse kufungia punda wake, karibu miaka 100 iliyopita.

Mnyororo ungalipo ingawa unazidi kumezwa na mmbuyu.

Hapa napo nikapata nafasi ya kukutana na Bi Selina.

Wakati naanza kazi Bagamoyo huyu ndiyo alikuwa Sekeretari wetu wa Idara ya Ushirika na maendeleo ya jamii, chini ya Mzee Mkodo na baadae Mujos


Kosa la Blogger, Olympus haikuwa na chaji ya kutosha..........

ikabidi Kinokia kichukue nafasi kupata taswira ya hili kanisa la awali kabisa ukanda huu wa Afrika Mashariki miaka zaidi ya 100 iliyopita
Hapa ndipo mwili wa Bw. Livingstone ulipolazwa wakati wa kusafirishwa toka Kigoma kupelekwa kwao.
mtaani nako Kinokia hakikukosa taswira.....

muda ulikuwa mchache, tulipaswa kugeuka mapema ili kuwahi mkutano wa wana ndugu uliokuwa unafanyika Kipunguni kwa Bw Eddyson

Wednesday, March 23, 2011

MDAU AMWAGA MSAADA KWENYE BLOG

Mdau Dr George jana baada ya kuwasili amekabidhi msaada wa Kamera ya kisasa kwa Admin wa Blog ya Msalya kama alivyokuwa ameahidi wakati wa safari yake iliyopita.

Ni OLYMPUS, Digital Camera VG-120/DE-705 toleo la January 2011

LEO NI SIKU YA MDAU MINOO

Leo tarehe 23 March ni BIrthday ya MDAU
AminaTereza Billy Kurwijira Msalya "Minoo"
HAPPY BIRTHDAY OUR DEAR AMINA

After 6 Yrs in Kagoshima, The Mdau George is Back

Mdau George na Familia yake amekuwa yuko nje ya nji kwa takribani miaka sita.
Na jana ilikuwa siku yake ya kurejea.
Wadau wa Dar walikuweko Eapoti kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ingawa ratiba kamili ilikuwa haijapatikana.
Baada ya kusubiria masaa, Kamera ya mdau ilinusa ndani ya arriving lounge na kunasa taswira hii ya wadau wakielekea geti la kutokea
Wadau wakakaa tayari........
Ikawa kunyanganyana kila mtu na wake.............
Aliyepata mtoto, haya...........
Aliyepata Mama, au mizigo haya..............................
Baada ya stori za hapa na pale, msafara ukaongoza chini ya ulinzi mkali ukifuatiliwa na kinokia kama kawaida
Hatimae msafara ukawasili Kipunguni, ambapo familia hii itapumzika japo kwa siku mbili tatu
Baada ya sara, stori zikaendelea................
huku kukiwa na lugha gongana, iliyoongozwa na Madame Pricilla

Monday, March 21, 2011

Enzi za Mid Nineties

Jumapili nyingine jana, pamoja na kuwauguza wagonjwa nyumbani, pekua pekua ikanikutanisha na picha za enzi hizo.
Ilipigwa Tabata..............
Likely 1995
Florah(Mama Jack), Chaibora na Mama Chai
Febronia aka febi, Late Mama Kilusungu, Penina na Mama Chai