Monday, November 29, 2010

PEKUA PEKUA

Jana kama kawaida ya jumapili ikawa siku yenye pilika nyingi.
Awali ilibidi niamuke mapema kuliko kawaida kumpa kampani Chief photographer wa Blog aliyekuwa akihama kutoka Ubungo kuelekea Kipunguni. na pia kujiandaa kwa kikao cha wana Ndugu kule kwetu Kinyerezi, mida ya alasiri.
Baada ya pilika pilika za hapa na pale, nikawa kwenye pekua pekua zangu za kawaida.
Na hizi hazikuhitaji Ki NOKIA tena

1995
Kadi ya wadau wakiomba michango ya sherehe ya Send Off
Mdau mmoja akanidokeza kuwa kati ya walioorodheshwa kupokea michango wakati huo,
Ni wawili tu sasa wangali hai.
Mola awalaze pema peponi Amina.

1997
Pekua pekua ikanikutanisha na kadi ya mwaliko wa mnuso wa wadau. Nakumbuka sherehe hii ilifanyika pale ambapo sasa ni drinking hall (kwa wadau wa River)
Lakini handwriting kama ya mdau George vile..................

2005
Kadi ya mwaliko wa mnuso
Vikao vikifanyika pale Nyambu Pub, kampani bab kubwa toka kwa Mr Machele wakati huo.
Kama kumbukumbu zinaenda vyema, bila shaka nilikuwa mwongozaji wa vikao hivi.

KILA LA KHERI WADAU

No comments:

Post a Comment