Total Pageviews

Monday, November 29, 2010

PEKUA PEKUA

Jana kama kawaida ya jumapili ikawa siku yenye pilika nyingi.
Awali ilibidi niamuke mapema kuliko kawaida kumpa kampani Chief photographer wa Blog aliyekuwa akihama kutoka Ubungo kuelekea Kipunguni. na pia kujiandaa kwa kikao cha wana Ndugu kule kwetu Kinyerezi, mida ya alasiri.
Baada ya pilika pilika za hapa na pale, nikawa kwenye pekua pekua zangu za kawaida.
Na hizi hazikuhitaji Ki NOKIA tena

1995
Kadi ya wadau wakiomba michango ya sherehe ya Send Off
Mdau mmoja akanidokeza kuwa kati ya walioorodheshwa kupokea michango wakati huo,
Ni wawili tu sasa wangali hai.
Mola awalaze pema peponi Amina.

1997
Pekua pekua ikanikutanisha na kadi ya mwaliko wa mnuso wa wadau. Nakumbuka sherehe hii ilifanyika pale ambapo sasa ni drinking hall (kwa wadau wa River)
Lakini handwriting kama ya mdau George vile..................

2005
Kadi ya mwaliko wa mnuso
Vikao vikifanyika pale Nyambu Pub, kampani bab kubwa toka kwa Mr Machele wakati huo.
Kama kumbukumbu zinaenda vyema, bila shaka nilikuwa mwongozaji wa vikao hivi.

KILA LA KHERI WADAU

Monday, November 22, 2010

KIKAO CHA NDUGU KUIMARISHA UPENDO

Jana tulikuwa na kikao cha ndugu wote waishio Dar Es Salaam, kule kweu Kinyerezi.
Lengo lilikuwa kuwaweka ndugu wote wa Dar es Salaam karibu katika Upendo na kuwa na mawasiliano thabiti na yenye uhakika.
Tayari kusaidiana kwa shida na raha.
Na kama kawaida, Ki Nokia kilikuwepo kunasa baadhi ya matukio.
japo kwa taarifa ya muda mfupi, waliohudhuria si haba, na tumeazimia tuwe na kikao kingine Jumapili ya tarehe 28/11 pale pale kwetu Kinyerezi.
Hususa sasa ni kuweka mambo sawa na ku "take off"
Mzee Mwayai alikuweko kutoa busara zake
seeing them off

Thursday, November 18, 2010

webcam test

IDD EL HAJI

Jana baada ya pilikapilika za sikukuu na mihangaiko ya hapa na pale, tukatoka hadi kule kipunguni kuangalia mizigo ya Marehemu Josia.
Baada ya tafakuri ya kipi kinaweza kwenda Bunda, kipi cha kubaki na kipi kifanyiwe nini. Hatimae tukafikia muafaka.
Katika safari ya kurejea kwetu Kinyerezi, tukasema si vibaya tukapitia Garden ku pass time.
Kwa wale mnaopajua KM Magereza, madhari yake ipo vizuri sana.
Kwa kuwa Ki Nokia changu nilikuwa nacho nikaona si haba nikanyaka japo picha mbili tatu za kumbukumbu.


VIJANA WA ENZI HIZO

Pekua pekua ya jana imenikutanisha na Picha hii.
Enzi za ujana wao.
Mwayai tulikuwa nae, anakumbuka ilipigwa studio moja mjini Mwanza kwenye miaka ya 1958.

Wednesday, November 17, 2010

LEO NI SIKUKUU

Leo ni sikukuu ya IDD EL HAJI,
Lakini leo pia ni
BIRTHDAY
ya mdau
MANYORI BILLY KURWIJIRA MSALYA
Picha hizi nimezipata asubuhi hii baada ya kuwa ameimbiwa
HAPPY BIRTHDAY
kwa kutumia Ki NOKIA changu kule kwetu Kinyerezi.
Naamini na wadau wengine pia mtaungana na wana Kinyerezi kumwimbia leo.
Katika Anniersary hii ya miaka 25
Lakini leo pia katika Kumbukumbu,
Inatimia miaka 25 toka mpendwa wetu
NYAMALELO BETTER KURWIJIRA MSALYA
alipotutoka kule Nkinga, Nzega.
DAIMA TUTAMKUMBUKA

Tuesday, November 9, 2010

BIRTHDAY YA MDAU - LILIAN


Katika pekua pekua yangu, nimekuta Mdau wetu wa Kagoshima keshokutwa anatimiza umri wa miaka kadhaa................................

TUMPE HONGERA ZAKE


Naamini ndugu zetu hawa watatuwakilisha kukuimbia

HAPPY BIRTHDAY OUR DEAR LILIAN


Wednesday, November 3, 2010

TASWIRA ZA UCHAGUZI KINYEREZI

Na hizi nilizinasa katika pita pita yangu hukuhuku kwetu.
Mlingoti mmoja kwa Bendera za wagombea wote.

Nilifanikiwa kuhudhuria ufunguzi wa Kampeni za udiwani kwa Kata ya kwetu Kinyerezi.
Bahati mbaya sikusikia sera zozote zenye kutia matumaini.

ADHA YA FOLENI ZA DAR






Juzi kati nikafanikiwa kupata taswira hizi za Foleni za Dar Salaam, hizi nilipata katika route ya Kinyerezi hadi Msimbazi mission Centre. Inakera umbali wa chini ya km 10 inakulazimu kutumia muda kati ya saa 1 hadi moja na nusu.