Monday, March 8, 2010

SIMULIZI ZA MZEE CK NA UKOO WA MSALYA


Simulizi hii inaanzia karibu miaka 200 iliyopita………………….
Hii imetoholewa kizazi kwenda kizazi na Bw. Seka Seka, na dadie Nyabhwangu Kisaka.

Simulizi inasema hivi
Zamani hizo, karibu miaka 200 iliyopita,
Bw. Manyori aliyekuwa akiishi sehemu za Sizaki alielekea sehemu za Bukwaya.
Huko Bukwaya Manyori alijaaliwa kukutana na Binti mmoja, ambae alikuja kuwa mke wake.
Jina hili limepotea kwenye kumbukumbu za msimuliaji.

Manyori na huyu mama kwa kumbukumbu zilizopo, walifanikiwa kupata watoto.
Idadi ya watoto hakuna uhakika sana, lakini watoto wawili wa kiume ambao kumbukumbu zipo ni Bw. Kisaka (Chisaka) na Kimori (Chimori).

Ukoo ukaendelea

Kisaka akamzaa Nyabhwangu na Nyesagi (mabinti hawa) kwa mkewe Mkoko

Kimori akamzaa Maseeme.

Miaka ikapita, Mzee Kisaka akafariki. Kwa taratibu za mila Bw. Maseme akaruhusiwa kumrithi mke wa Kisaka (Baba yake mkubwa), Bi Mkoko au Nyakagere.

Maseme kwa mke wa Kisaka(Bi Mkoko) wakawazaa Msalya na Nyalimbi.

Hebu tutafakari hapa kidogo,
Nyabhwangu na Maseme ni Dada na Kaka (kwa baba mkubwa na mdogo)
Msalya na Nyalimbi ni wadogo zake na Nyabhwangu (mama mmoja)
Msalya na Nyalimbi wanae Maseme (Hakika damu yake)
…………basi pia Nyabhwangu ni shangazi yake Msalya………….


Maisha yanaendelea ukoo unaendelea

Maseme alifariki akimwacha Msalya akinyonya, Mama yake na Msalya baada ya kifo cha mumewe, alihama kutoka Bukwaya kwenda kuishi sehemu za Kisorya eneo la Nambubhi. Enzi hizo ikiwa katika utawala wa Ukerewe, wilaya ya Mwanza mkoa wa Lake Province.
Lake Province sasa ndiyo Kagera, Shinyanga, Mwanza na Mara kwa pamoja.

Nyabhwangu kwa mume wa kwanza wa Ukerewe akamzaa Mnyaga.
Baadae kwa mume wa pili wa Kiruli akawazaa Manoko, Muruguta na Nyamakale.

Nyalimbi akawazaa Kalyanja, Nyamumwi na Nyanyama

Msalya kwa wakeze tofauti akawazaa Bhajalaki, Manyori, Kurwijira, Mwayai, Nyanjula, Gabhaseki, Chabhusiku, na Taabu.
Msalya aliishi na kukulia Kisorya Nambhubi. Watoto Bhajalaki, Manyori, Kurwijira, Mwayai, Nyanjula wamezaliwa hapo. Baadae kwenye mwaka 1937 alihama kuelekea Kitengule, eneo panapojulikana zaidi sasa kama Nyakatubha. Hapa ndipo watoto wake Gabhaseki, Chabhusiku, na Taabu walizaliwa. Msalya alikaa eneo hili hadi alipofariki mwaka 1966.

Kwa upande wa pili, Bibi (Nyanya) yake Msalya alitokea Kisiwa cha Ukara, akaolewa huko maeneo ya Bukwaya na Bw. Kagele. Miongoni mwa watoto wao ni Binti yao aliyeitwa Mkoko (jina la kuzaliwa) lakini akijulikana zaidi kama Nyakagele kwa kutumia jina la Baba.

Kumbukumbu zinazopatikana, Kagele amezaliwa pamoja na Kaka yake akiitwa Kwesi na akiwa na mdogo wake akiitwa Lugeji.

Kwesi akamzaa Mgole.

Mgole akiishi pale eneo la Kasahunga nae akawazaa Kwesi na Mkwaji.
Kwesi Mdogo akimzaa Mkumbya, Ebunda, Kagere, Lyanga na wadogo zao wa kike.
Lugeji hakubahatika kupata motto.


Next time nitawaletea matawi yanayoendelea
Family tree…………………………

3 comments:

  1. ukoo umetulia, ila nimegundua majina mengine nilikuwa nayasikia tu sikujua walikuwa na uhusiano hgani. Majina kama Kwesi, Mnyaga n.k. kumbe jamaa wametoka mbali. Vipi hakugusa yule Msalya Mudavadi wa Kenya nasikia wana asili ya Ethiopia hawa ni kweli?

    Mdau,
    Kagoshima

    ReplyDelete
  2. Sosi wa Gongo la Mboto ni mtoto wa Lyang'a, sasa angalia connection na Msalya, lakini mama yake Nyakataga ni mpwa wa CK, huko nako kunahitaji maelezo ili kueleweke vizuri.
    Maelezo yaanze kwa Bituro, Sarah nk

    posted by nyachiriga bright msalya

    ReplyDelete