Total Pageviews
Tuesday, December 28, 2010
Friday, December 24, 2010
Monday, December 20, 2010
ILIKUWA WIKI YA PILIKA NA KUMBUKUMBU
IJUMAA
17.12.2010
Mheshimiwa wa Halmashauri alitunukiwa leseni ya Uwakili na Serikali.
Safari ya Sheria ndio imeanza.
HONGERA NYACHIRIGA
JUMAMOSI
18.12.2010
Pilika pilika zikalazimisha kuvuka bahari kwenda Kigamboni, wengine tukaingia foleni ya masaa matatu.
Huko,
Mdau Lulu Bright Msalya alikuwa akilamba Nondozzz yake ya kwanza ya Siasa, Sayansi na Maendeleo ya jamii toka Mwalimu Nyerere Academy
19.12.2010
Pilikapilika zikaanzia Ubungo Terminal
Wadau Mr & Mrs Mwayai Msalya Baada ya ziara ya kuzuru kaburi la mdau Josia walikuwa wakikwea pipa "NAJMUNISA COACH" kurejea Bunda
SAFARI NJEMA
Wadau wa Kule Kinyerezi wakapata nafasi ya Kumwimbia HAPPY BIRTHDAY ya miaka 17
Mdau SARAH BILLY MSALYA
Ki Nokia hakikuweza kunasa kwa kuwa hakikuwa na mwanga wa kutosha
Ki Nokia kikafufuka
Kikamnasa mdau alieamuka alfajiri kwa ajili ya kufanya usafi.
Leo ni BIRTHDAY yake ya NANE
Thursday, December 2, 2010
NYAMWEYA DAY 12.12.2010
Wadau wa Mwanza, Bunda, Geita na kwingineko naamini watakuwa mkao wa kuondoka.....
Monday, November 29, 2010
PEKUA PEKUA
Awali ilibidi niamuke mapema kuliko kawaida kumpa kampani Chief photographer wa Blog aliyekuwa akihama kutoka Ubungo kuelekea Kipunguni. na pia kujiandaa kwa kikao cha wana Ndugu kule kwetu Kinyerezi, mida ya alasiri.
Baada ya pilika pilika za hapa na pale, nikawa kwenye pekua pekua zangu za kawaida.
Na hizi hazikuhitaji Ki NOKIA tena
1995
Kadi ya wadau wakiomba michango ya sherehe ya Send Off
Mdau mmoja akanidokeza kuwa kati ya walioorodheshwa kupokea michango wakati huo,
Ni wawili tu sasa wangali hai.
Mola awalaze pema peponi Amina.
1997
Pekua pekua ikanikutanisha na kadi ya mwaliko wa mnuso wa wadau. Nakumbuka sherehe hii ilifanyika pale ambapo sasa ni drinking hall (kwa wadau wa River)
Lakini handwriting kama ya mdau George vile..................
Kadi ya mwaliko wa mnuso
Vikao vikifanyika pale Nyambu Pub, kampani bab kubwa toka kwa Mr Machele wakati huo.
Kama kumbukumbu zinaenda vyema, bila shaka nilikuwa mwongozaji wa vikao hivi.
Monday, November 22, 2010
KIKAO CHA NDUGU KUIMARISHA UPENDO
Lengo lilikuwa kuwaweka ndugu wote wa Dar es Salaam karibu katika Upendo na kuwa na mawasiliano thabiti na yenye uhakika.
Tayari kusaidiana kwa shida na raha.
Na kama kawaida, Ki Nokia kilikuwepo kunasa baadhi ya matukio.
Hususa sasa ni kuweka mambo sawa na ku "take off"
Thursday, November 18, 2010
IDD EL HAJI
Baada ya tafakuri ya kipi kinaweza kwenda Bunda, kipi cha kubaki na kipi kifanyiwe nini. Hatimae tukafikia muafaka.
Katika safari ya kurejea kwetu Kinyerezi, tukasema si vibaya tukapitia Garden ku pass time.
Kwa wale mnaopajua KM Magereza, madhari yake ipo vizuri sana.
Kwa kuwa Ki Nokia changu nilikuwa nacho nikaona si haba nikanyaka japo picha mbili tatu za kumbukumbu.