Total Pageviews

Thursday, November 12, 2015

SIMULIZI ENDELEVU YA UKOO WA MSALYA



Nilipata zamani zile
Jumatatu Tarehe 8, Machi 2010 kuwapakulia hapa simulizi za ukoo wa Msalya. Simulizi hizo zikitoholewa na Mzee CK.
Mwezi wa Agosti mwaka huu nilirejea huko Nakatuba katika kikao cha ukoo, kilichoendana na kumbukumbu ya takribani mwaka mmoja toka alipotutoka Mzee CK.
Mzee Mwayai aliongoza tena hizi simulizi endelevu akisaidiana na ndugu zake.

..........ungana nami  tena leo kwenye mwendelezo wa simulizi hii ya ukoo wa  MSALYA.........

MSALYA 1895 – 04 Juni 1966.
Msalya kama alivyokuja kujulikana baadae, alipozaliwa aliitwa jina la Babu yake mkubwa Chisaka. Wengi wanalihusisha jina la Msalya na uoaji wa Wake wengi mmoja baada ya mwingine.
Wakeze Msalya ni pamoja na:
Myango: Mama yake Bhajaraki na Manyori
Bhituro: Mama yake Kulwijira na Mwayai
Bhuinda (Nyamusibha): Mama yake Nyanjura
Nyamata: Mama yake Gabhaseki
Kamwanyi (Amefariki 2013): Mama yao na Chausiku, Tabhu na marehemu Daudi
Mwananonga: Mke wake wa mwisho, ambae hawakujaaliwa kupata watoto  mwenyeji wa Tabora.

Msalya kwa upande wa ndugu, alikuwa na kaka yake akiitwa Nyachiriga. Na pia amezaliwa na dada zake Nyabhwangu, Nyalimbe na Nyaswi.
Nyabhwangu ni dada yake Msalya kwa kuzaliwa na mama mmoja, Bi Mkoko. Ingawa pia kwa upande mwingine ni shangazi yake kwa sababu Nyabhwangu Chisaka ni dada yake Maseme (Baba wa Msalya).

Nyalimbe ndiye mama yao  Karyanja (Mrs Mjengwa au Mama Msiba), Nyamumwi (Mama yake Jangu) na Nyanyama (Mrs Maryanyo au Mama Remi).
Nyabhwangu aliwazaa Mnyaga kwa mme wa kwanza, na mme wa pili akawazaa Manoko, Muruguta, na Nyamakale.
Nyamakale ndie mama yao John na Heri Ndaro.

Nyaswi yeye aliwazaa Nyakobhe na Nyangeta.

Ndugu wengine wa Msalya wanaojulika pia kwa upande wa baba ni pamoja na:
Kwesi: Baba yao Mbulawabho(Mama yake Pamba Mfungo), Kwebheta na Makene
Magesa: Baba yake Masua na ndugu zake
Chausi: Baba yake Goodluck



...............tutaendelea .....................

Tuesday, November 10, 2015

NI SIMANZI.......

Bi Grace, Mama wa watoto waliofariki.
 Mazikoni, Makaburi ya Kingolwira Morogoro.
 Hapa ndipo walipopumzishwa wapendwa wetu Christina, Musheri na David
Waombolezaji wakirejea toka mazikoni
Bw. Kenedy. Baba wa marehemu
Huyu ndiye aliyenusurika katika mkasa huu.
Marehemu Christina
                                                                Marehemu Musheri
                                                           Marehemu David Mafuru
Jumamosi ya tarehe 07 Novemba 2015 ikianza vyema asubuhi, lakini ikiiacha familia ya Bw Kennedy na Bi Grace ikiwa na machungu na majonzi ya kuondokewa na watoto wao watatu kwa ajali ya kuzama kwenye dimbwi la maji.
Asubuhi hiyo Grace na wanae hawakwenda kanisani kama ilivyo kawaida yao, badala yake Grace aliondoka nyumbani maeneo ya mashambani, Mikese Morogoro kwenda kumjulia hali wifi yake maeneo ya Kingolwira, Morogoro.
Bw Kennedy nae katika kuhakikisha maisha yanasonga, akakodi Bodaboda kwa ajili ya kupeleka mikungu yake ya ndizi eneo la Mikese Mizani kwa ajili ya kuuza.
Watoto baada ya kuachwa nyumbani peke yao, katika michezo yao iliwafikisha maeneo ya mabondeni kwenye majaruba ya mpunga. Hapa ndipo walipopatwa na wazo la kuingia majini kuogelea.
Watatu waliingia majini kuogelea, na huo ndio ulikuwa mwisho wao.
Mmoja mdogo hakuingia majini alibakia na mavazi ya ndugu zake, na huo ndio ulikuwa uzima wake.
Mtoto huyu alikutwa na wapita njia, na katika kumhoji kutaka kujua kulikoni ndipo ikaja kudhihirika kuwa ndugu zake wengine watatu walikuwa wamezama majini, wamefariki dunia.
Hii ilikuwa mida ya asubuhi kwenye saa nne.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

Friday, November 6, 2015

GARI HAIJAI

Gari haijai, inajaa ndoo ya maji.
Ndio msemo wa huku kwetu.
Mtabanwa, mtashindiliwa 
lakini wote mtaingia.
Njiapanda kwetu, asubuhi.

Wednesday, November 4, 2015

PHOTO SHARING FROM LAMADI

New Nezia, "Mama Mkwe" 
Jabaman 
CK Junior
All with Love from Lamadi 

NDIO ZETU

Baada ya wiki moja ya barabara kuwa tupu wakati wa kusubiria matokeo ya uchaguzi mkuu, mambo ya foleni yameanza kama kawaida yake wiki hii.
Njiapanda ya Segerea leo asubuhi. 

HAKUNA AJUAE

Hakuna ajuae,
Mzima kuwa mfu, mgonjwa kuwa salama.
Tazara asubuhi. 

HATA WAO WANAWEZA

Siyo lazima kuwezeshwa,
Wamama ukiwapa lift wanaweza.
Kawawa Rd