Total Pageviews

Wednesday, November 16, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - MAJITA (1)

Day 13 ya vekesheni ikaendelea kwa mwelekeo wa njia ya Majita.
Stop over Bukima
Mji mkongwe katika kanda hii ya majita, lakini ukuaji wake unaonekana ni wa kusuasua.
ni tofauti na enzi zile za Mali ya Umma alipokuwa anavuma.
Makojo ilikuwa kituo chetu cha kwanza.
Heshima pahala alipopumzika Shangazi Ghabhaseki Msalya na Mmewe Mafuru Nyabhyuga.
Wazazi wa Tatu, Gasige,Bhulesi,Siri,Daniel,Adamu, Grace, Msalya, Taabu na Salya.
RIP Aunt

Tukipokewa kwa bashasha na mwenyeji wetu Mr Gasige na familia yake

Timu yangu ikajaribiwa kuukwea Mlima Kilimanjaro

Na ndani ya muda mfupi msafara wangu ukiwa na wataalamu kama CK Jnr 2, na wengineo mlima Kilimanjaro haukuwa ni chochote mbele yetu

Ilikuwa furaha kuwa pamoja na familia hii japo kwa muda mfupi kwani safari ilikuwa haina budi kuendelea



Bhulinga,

Nyamagoti akiwa hajajua kinachoendelea kuwa msafara ulikuwa tayari uko kwake

Alipopumzika Mugerera Phares Chisute Mteki (1957 -2006)

RIP Phares

Furaha mnapokutana baada ya miaka mingi kupita, utatamani muda usimame japo kwa sekunde
Ikawa wakati wa kupeana habari za hapa na pale

Mama Mgerera na Bhikara (Baba Mwenye nyumba)
Chisute Mteki na Nyamagoti

simulizi kedekede, na utambulisho kwa wasiofahamiana.
Baraka zikajazwa kwenye chombo chetu cha safari

Picha ya kumbukumbu ilipopatikana chance ya kufanya hivyo
Lakini hatimae ilikuwa ni wakati wa kuwaona wageni wao wapendwa wakiondoka. Ilibakiana kutakiana heri na baraka kwamba Mungu atujaalie tukutane tena safari nyingine.

Monday, November 14, 2011

WATU BILION SABA DUNIANI - MAMBO SABA YA KUSTAAJABISHA

Kutoka www.cbsnews.com
Dunia imefikia hatua kubwa: Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa idadi ya watu duniani walivuka bilioni saba ilipotimu usiku wa manane wa tarehe 31 Oktoba 2011.
Kwa bahati mbaya, bilioni saba si sababu ya msingi ya kusheherekea, kwani ongezeko la zaidi la watu laweza kuleta matatizo zaidi.

Ulimwengu haujawahi kuwa na watu wengi zaidi. Tunaongezeka milioni 80 kila mwaka, sawa na idadi ya watu Ujerumani. Lakini kiwango cha ukuaji kwa dunia yetu kinaporomoka.Mwaka 1950 wastani wa watoto kwa kila mwanamke ilikuwa watano, Lakini leo ni watoto 2.5 kwa kila mwanamke.

Katika baadhi ya nchi, kiwango cha chini ya kuzaliwa ni tatizo. Nchini Italia, kwa mfano, wastani wa watoto kwa kila mwanamke ni 1.2, chini ya kiwango, hii ina maana miaka ijayo wazee watakuwa wengi kuliko vijana.

Watu Bilioni saba siyo tatizo kuhusiana na nafasi, Kama kila mtu katika ulimwengu wangesimama bega kwa bega, tungeweza kuenea ndani ya mipaka ya jiji la Los Angeles.

Hakuna mtu duniani anaepaswa kufa kwa njaa.Kwa mfano mwaka jana dunia ilizalisha chakula tani bilioni 2.3 za nafaka za kutosha kulisha watu bilioni 9 hadi 11. Hata hivyo, tatizo ni kuwa asilimia 46 tu ya kiasi huenda vinywani mwa binadamu na kinachobakia hulishwa wanyama hasa wale waliwao na hivyo kusababisha watu bilioni moja kushinda na njaa kila siku.
Kama idadi ya vegans ingeongezeka, basi dunia ingejitosheleza kwa chakula.

Mzigo mkubwa kwa rasilimali duniani.Si sana kuhusu idadi ya watu, kama ni idadi ya kaya. Kama ilivyo kwa Watu sita wa kaya moja kutumia jokofu moja hutumia nishati pungufu kwa kila mmoja ukilinganisha na watu sita kila mmoja akitumia jokofu lake.

Elimu ni kigezo kikubwa katika kudhibiti ongezeko la watu.
Vijana wanapokuwa shule muda mrefu, huchelewa kuoa/kuolewa na hivyo kuchelewa kuanza
kupata watoto. Na pia wanapoelimika hupendelea kupata idadi ndogo ya watoto.

Katika dakika tatu tu, watu 900 wanazaliwa, watu 360 wanakufa, na dunia inakuwa na ongezeko la watu 540.

Friday, November 11, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - KARUKEKERE

Nyamweya Rebecca RIP(1913 - 20 December 2002)
Vacation ilinipeleka Karukekere.
Kuzuru pahala alipopumzika Bi Mkubwa Rebecca Nyamweya na mwanae na mjukuu wake.
kama kawaida nikawa na kampani ya kutosha.


Wadau Joshua na CK Jnr2, wao walikuwa na namna tofauti ya kuzuru makaburi haya

Mrs Nezia M. Magoti
Ni furaha sana tunapokutana na ndugu baada ya kuwa mbali muda mrefu.

Bi wakubwa wakapata nafasi ya kuteta mambo yao

Nyamkaruka

Masururi,
Kwa Bi mkubwa Lusia


bila ya shaka akimwambia " Umekuwa mkubwa hivi..................."

Nani alisema huku kwetu hakuna mambo ya mitandao???

Uncle Muyabhi, hakutaka kupigwa picha

Lakini pamoja na kuruka ruka, hakuweza kabisa kukwepa lens za kamera za blogger

Nikiwa karukekere nilikutana na Bw Mabhanga Makaranga, miaka 33 tokea tulipoachana Mara secondary. Maisha si mchezo, sikuweza kupata picha yake.

Kupoza kiu, maji baridi ya mtungi wa kwetu

ni wakati wa kubarizi na kupeana habari za masiku tele.
Masururi, Beria, Macklaude, Bi Penina

Mrs Bilshani"Chuma",Bi Penina, Bi Tereza, Mashaka

Mrs Cecilia Macklaude na wageni wake









Kwetu hakuna haja ya viyoyozi

Safari yetu ya kurudi tulipitia kumwona ndugu yetu, Bw Mganji anaesumbuliwa sasa na matatizo ya miguu
ugeni ukapokelewa kwa bashasha na wenyeji

Mr Mganji

Bi Mkubwa Tabitha Malekela (Mrs Mganji)