Total Pageviews

Wednesday, October 20, 2010

MDAU TABI NA SAFARI YA MAJUU

Kabla ya safari ya kukwea Pipa, Mdau alifika kwa Ankal Kule nyumbani kwetu Kinyerezi kupata angalau dua, na mkono wa baraka na kwaheri
Konoz la safari njema
Wadau wakawepo safari ya usindikizaji pale Mwl Nyerere Airport ya uwanja wa Ndege
wadau kutoka MORO, Mji kasoro bahari walikuwepo kuweka baraka zao
mdau akatafakari, huyu Mama keshaondoka .......kilichobaki
Nipotezee.............................
Eeh, Lakini..................
Hivi ndege yao ndiyo ile kule juu....................
SAFARI SIO KIFO, TUTAONANA..............

KALALE PEMA MDAU, KAMANDA JOSIA MSALYA


Mipango ya malazi ya mwisho ya Mdau Josia Mwayai Msalya, yakiendelea. Ni pale nyumbani kwetu Kinyerezi, Ukonga, Ilala Dar Es Salaam

Wadau, washiriki na viongozi wa kanisa la SDA Ubungo Hill walijumuika, na kutoa neno

Kwaya ya SDA Ubungo Hill, ilitoa ujumbe wa kututaka kujiandaa wakati wote kabla ya safari

Wazee wa Kanisa walitoa hekima zao katika kumtukuza Mungu

Wasifu wa Mdau ukawekwa bayana,

Mchamungu, mwenye msimamo na aliyekuwa tayari kusimamia lile analoliamini.

KWAHERI MDAU JOSIA

........Malembo...............

...........Aznati...............

Kwaheri Baba, kamsalimie Mama....







Ulitoka kwenye Udongo, utarudi kwenye udongo

Friday, October 15, 2010

ENZI ZILE ZA MDAU WA MTWARA


Juzi Mudau wa Mtwara katika kufanya fanya usafi kwenye Library yake kakumbana na Photo moja maridadi sana ya enzi hizo. Katika kukumbuka kumbuka ikaonekana imepigwa before nineties, wakati huo mdau alikuwa akijiandaa kukwea pipa kwa safari ya masomo huko The Netherland. Tunakupongeza mdau kwa utunzaji huo wa kumbukumbu ya enzi hizo.

Naamini utatupa na maelezo zaidi kuhusiana na picha hii.
ilipopigwa, wadau pichani, waliko sasa na dodoso nyingine kama zipo.........

Wadau wote zile picha za Mzee Ck zilizokuweko kule nakatuba ziko wapi???????????
alipenda sana kupiga picha na familia. Mwenye kuwa nazo tunamkaribisha azirushe kwenye blog.

Monday, September 27, 2010

TANZIA - JOSIA MWAYAI MSALYA 1971 TO 26.09.2010

Josia Mwayai Msalya
1971 to 26.09.2010

Mpendwa wetu amefariki jana majira ya saa nane na robo nyumbani Kinyerezi, Dar Es Salaam.

Tunataraji Mazishi yatafanyika siku ya Jumanne tarehe 28 September 2010 majira ya saa kumi alasiri makaburi ya Kinyerezi Dar Es Salaam.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake libarikiwe.

AMINA


Friday, September 24, 2010

HAPPY BIRTHDAY MDAU EDDY

MDAU HUYU ALIZALIWA TAREHE 20 SEPTEMBER 19........, SAA 9.30 ALASIRI HUKO KISORYA BUNDA.
Makala na mitandao mbalimbali imekuwa ikionesha tarehe tofauti tofauti za kuzaliwa mdau.
Blog imefuatilia na kupata uhakika wa tarehe
Na mdau alipobanwa na Blog, alikiri kunyuti........................

HATUJACHELEWA SANA KUMPA STAHILI YAKE!!!!!!!!!
Chief Photographer wa Msalya Blog

HAPPY BIRTHDAY OUR DEAR MNYAGA EDDYSON
HAPPY BIRTHDAY TO UUUUUUUUUUUUUUUU

Saturday, September 18, 2010

REBECCA NYAMWEYA DAY 12 DECEMBER 2010

Picha ya Nyamweya mwishoni mwa miaka ya 90 kama sikosei.
Alifariki mwaka 2002 akiwa ameshavuta zaidi ya miaka 95.
Katika kumukumbuka mtu huyu muhimu sana kwetu, na katika kujaribu kutunza kumbukumbu yake kwa kina Rebeca wajao, Mwalimu Maclaud anaandaa siku maalum ya REBECA NYAMWEYA siku ya tarehe 12.12.2010 huko KARUKEKERE.
Wajukuu wote wanatakiwa kuweko huko wakiwa na familia zao zote.
Watu wote wanashauriwa kuandaa usafiri wao binafsi, angalau kuwepo Karukekere siku moja kabla.

Kutakuwepo na kongamano na maelezo kutoka kwa watu waliokaa na Rebecca na kufahamu historia yake.
Mmepata kusikia kusikia jinsi alivyokutana na waume zake, Magoti I na Magoti II.

Nafasi yako kati ya nafasi adimu zipatikanazo kuhifadhi kumbukumbu hii.
Picha hii ilipigwa na Magoti III