Total Pageviews

Thursday, June 3, 2010

FROM MWANZA TO NAKATUBA ON VEKESHENI

kwa mtiririko mzuri wa matukio, ni vyema ukaanza picha ya chini, kwa kupanda juu.
Sorry for Incovinience, ilitokana na matatizo ya kimtandao kidogo.
Na hatimae kulikuwa na picha ya Ukumbusho huu......................
Naamini Vekesheni hii itabakia kumbukumbu safi kwa muda mrefu kwa vizazi vya kina Pricilla
Kumbe wageni hawakuja mikono mitupu.....
Walikuja na Zawadi kibao.
Bi Penina alikuwa miongoni mwa waliojimwayamwaya na mizawadi kibao
Wenyeji walipopata nafasi, walikaa nakupumua kidogo............
Hata kikombe cha Chai sasa ilikuwa ruksa kupita
Ilipopatikana chance, watu walipeana habari za mjini na za shamba
Wakabadilishana mawazo.............
Maneno mazuri ya busara huwa hayakosekani wakati huo.
Kila mmoja alihakikisha anatimiza wajibu wake ili kufanya mambo yende sawa, na ilipobidi wengine waliitana chemba na kuteta kidogo....................
Mahanjumati kama kawaida, kuwaacha wageni wakiwa na furaha tele, tele .....
Bi Mukima, Bi Penina na Bi Nyamisi walikuwepo standby kuwapokea wageni kutoka Mwanza,
Wageni hao wanaingia................................................



































PLANNED NAKATUBA VEKESHENI


Wadau wamepania kufanikisha Vekesheni ya Nakatuba panapo mwezi wa Saba.
Mipangilio hii iwe babu kubwa kulikoni ile ya CK 55 yrs of nanihii.............
Hii ni ya Mwenyewe Dingi, Msalya Senior.
.............to 1966.
Hapa mdau mwakilishi wa Dar akijaribu kutayarisha itenerary ya safari nzima, ikiwa ni pamoja na ukadiriaji wa gharama za safari kwa ajili ya vekesheni hiyo.
Duh!!!
Wadau wametakiwa kuhakikisha wanajiandaa vilivyo,kwani kiasi cha chini cha kuweza kukamilisha Vekesheni yenyewe ni kama m4 kasoro ushee kidogo.
Lakini sina shaka, maana wadau wa kusini kule wamepania kikweli...
Na central nako ndio usiseme.
Lazima twende pamoja

Monday, March 8, 2010

KUMBUKUMBU YA VEKESHENI


Katika kupitia pitia nikakutana na picha ya zamani zile...
Ilikuwa kama Vekesheni vile.
Ilikuwa safari ya Nakatuba,
Dada mmoja anajiandaa kupata Mwenza.........
Tukasema tukampe Kampani
Hapa tunakaribia kijijini, tukaambizana maji yetu haya ya kizungu kizungu hayafai huko vijijini, hivyo tupige mafunda mawili chap chap tuanze.
Chupa itawafaa kwa kuchukulia mafuta ya Taa.
Ni pale kilima cha Manana.
Enzi tunakua, thubutu kama kulikuwa na mtu ana ubavu wa kufika hapa na kupumzika vile na kupiga picha.
Kuanzia shoto Blogger mwenyewe, Penina na Lulu

SIMULIZI ZA MZEE CK NA UKOO WA MSALYA


Simulizi hii inaanzia karibu miaka 200 iliyopita………………….
Hii imetoholewa kizazi kwenda kizazi na Bw. Seka Seka, na dadie Nyabhwangu Kisaka.

Simulizi inasema hivi
Zamani hizo, karibu miaka 200 iliyopita,
Bw. Manyori aliyekuwa akiishi sehemu za Sizaki alielekea sehemu za Bukwaya.
Huko Bukwaya Manyori alijaaliwa kukutana na Binti mmoja, ambae alikuja kuwa mke wake.
Jina hili limepotea kwenye kumbukumbu za msimuliaji.

Manyori na huyu mama kwa kumbukumbu zilizopo, walifanikiwa kupata watoto.
Idadi ya watoto hakuna uhakika sana, lakini watoto wawili wa kiume ambao kumbukumbu zipo ni Bw. Kisaka (Chisaka) na Kimori (Chimori).

Ukoo ukaendelea

Kisaka akamzaa Nyabhwangu na Nyesagi (mabinti hawa) kwa mkewe Mkoko

Kimori akamzaa Maseeme.

Miaka ikapita, Mzee Kisaka akafariki. Kwa taratibu za mila Bw. Maseme akaruhusiwa kumrithi mke wa Kisaka (Baba yake mkubwa), Bi Mkoko au Nyakagere.

Maseme kwa mke wa Kisaka(Bi Mkoko) wakawazaa Msalya na Nyalimbi.

Hebu tutafakari hapa kidogo,
Nyabhwangu na Maseme ni Dada na Kaka (kwa baba mkubwa na mdogo)
Msalya na Nyalimbi ni wadogo zake na Nyabhwangu (mama mmoja)
Msalya na Nyalimbi wanae Maseme (Hakika damu yake)
…………basi pia Nyabhwangu ni shangazi yake Msalya………….


Maisha yanaendelea ukoo unaendelea

Maseme alifariki akimwacha Msalya akinyonya, Mama yake na Msalya baada ya kifo cha mumewe, alihama kutoka Bukwaya kwenda kuishi sehemu za Kisorya eneo la Nambubhi. Enzi hizo ikiwa katika utawala wa Ukerewe, wilaya ya Mwanza mkoa wa Lake Province.
Lake Province sasa ndiyo Kagera, Shinyanga, Mwanza na Mara kwa pamoja.

Nyabhwangu kwa mume wa kwanza wa Ukerewe akamzaa Mnyaga.
Baadae kwa mume wa pili wa Kiruli akawazaa Manoko, Muruguta na Nyamakale.

Nyalimbi akawazaa Kalyanja, Nyamumwi na Nyanyama

Msalya kwa wakeze tofauti akawazaa Bhajalaki, Manyori, Kurwijira, Mwayai, Nyanjula, Gabhaseki, Chabhusiku, na Taabu.
Msalya aliishi na kukulia Kisorya Nambhubi. Watoto Bhajalaki, Manyori, Kurwijira, Mwayai, Nyanjula wamezaliwa hapo. Baadae kwenye mwaka 1937 alihama kuelekea Kitengule, eneo panapojulikana zaidi sasa kama Nyakatubha. Hapa ndipo watoto wake Gabhaseki, Chabhusiku, na Taabu walizaliwa. Msalya alikaa eneo hili hadi alipofariki mwaka 1966.

Kwa upande wa pili, Bibi (Nyanya) yake Msalya alitokea Kisiwa cha Ukara, akaolewa huko maeneo ya Bukwaya na Bw. Kagele. Miongoni mwa watoto wao ni Binti yao aliyeitwa Mkoko (jina la kuzaliwa) lakini akijulikana zaidi kama Nyakagele kwa kutumia jina la Baba.

Kumbukumbu zinazopatikana, Kagele amezaliwa pamoja na Kaka yake akiitwa Kwesi na akiwa na mdogo wake akiitwa Lugeji.

Kwesi akamzaa Mgole.

Mgole akiishi pale eneo la Kasahunga nae akawazaa Kwesi na Mkwaji.
Kwesi Mdogo akimzaa Mkumbya, Ebunda, Kagere, Lyanga na wadogo zao wa kike.
Lugeji hakubahatika kupata motto.


Next time nitawaletea matawi yanayoendelea
Family tree…………………………

Monday, February 8, 2010

HAYA NDIYO MAVUNO YA 2009

mabibo hostel, Ubungo Dar Es Salaam
Vijana wetu hawa wanayomatumaini ya kufika hapa................

Hali halisi ya Nchi nzima kwa matokeo ya form Four 2009 ilikuwa hivi


DIV One to Three Watahiniwa 42,672 sawa na 17.85%

DIV Four Watahiniwa 130,651 sawa na 54.66%

Div Zero Watahiniwa 65,708 sawa na 24.49%


KAZI KWELIKWELI IKO MBELE YA WALIMU WETU TANZANIA


Mwalimu Belly, Mwalimu Msalya, Mwalimu Bilshani, Former Mwl Bright, Former Mwalimu Sarah......

Na jamii nzima ya Tanzania



S1383 MZINGA SECONDARY SCHOOL
DIV-I = 0 DIV-II = 3 DIV-III = 15 DIV-IV = 81 FLD = 24
S1383/0022 F NEEMA B MSALYA 29 IV CIV-D HIST-D GEO-D KISW-C ENGL-D BIO-F B/MATH-F


S0316 KIBASILA SECONDARY SCHOOL
DIV-I = 8 DIV-II = 35 DIV-III = 77 DIV-IV = 193 FLD = 87
S0316/0170 F PENINA BILLY 30 IV CIV-D HIST-D GEO-F KISW-C ENGL-D BIO-F B/MATH-F


P2517 ALFA SECONDARY SCHOOL CENTRE
DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 5 DIV-IV = 458 FLD = 248
P2517/0465 M BAASHA M MSALYA 32 IV CIV-F HIST-D GEO-F B/KNOWL-D KISW-D ENGL-F LIT ENG-F B/MATH-F


P0359 KIGURUNYEMBE SEC. SCHOOL CENTRE
DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 0 DIV-IV = 307 FLD = 322
P0359/0043 F BITURO T MSALYA - IV CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-D

Tuesday, February 2, 2010

TUKIKUMBUKA NYUMBANI

Nyumbani kwetu, enzi hizo
Furu, Ngobhegophe, mbete, nyingu, soga, etc etc.................................
Na baadae baba lao Sangara
Miss them a lot.

Thursday, January 28, 2010

Unaijua Familia ya Duggar

Familia ya Bw. Jim & Bob Michelle Duggar
Familia hii ya wacha Mungu ina watoto 18 na mjukuu mmoja.
Wanataraji kupata mtoto mwingine panapo mwezi wa tatu 2010.
Mungu anawabariki sana
----------------------------------
Jim Bob & Michelle Duggar & Family
Enjoying First "GrandDuggar" Mackynzie while awaiting baby 19 arrival!
Our new grand-daughter Mackynzie Renée is here! She was born October 8, 2009 to our oldest son Josh and his wife Anna! We are so grateful for this new grand-addition to our family and the Aunts and Uncles are so excited for
Josh & Anna! Our 19th child is due to arrive around March 18, 2010! We are enjoying this new phase of life as grandparents, while at the same time looking forward to the arrival of our next little one!
Psalm 127 says, “Lo children are a heritage of the Lord, the fruit of the womb is His reward.” We believe that each child is a special gift from God and we are thankful to Him for each one.