Total Pageviews

Wednesday, November 8, 2017

ZEBRA CROSSING

Zebra Crossing,
Kivuko cha Barabarani kwa ajili ya waenda kwa Miguu.
Maarufu kwa nakshi yake ya Mistari Mieupe na Mieusi, mithili ya Punda Milia.
Kikilenga kuwa pahala salama pa kuvukia waenda kwa Mguu Duniani kote.
Lakini Je?
Madereva wetu wanaheshimu......
Vingunguti, Barabara ya Nyerere
Jumanne jioni.

KAMONGO

Mzigo umewasili,
All the way from Nakatuba,
Kamongo the Fish.

Tuesday, November 7, 2017

USWAZI KWETU

Uoto wa kijani unarejea baada ya siku chache za Mvua,
Bob, Wifi, Dizzo na Potta wanasherekea.

UTII BILA SHURTI!!

 Umekaa kwenye Foleni muda sasa,
Lakini anatokea Dereva wa Daladala asiye Muungwana,
Hawezi kutii sheria bila Shurti.
Yeye ana haraka zaidi............
Segerea Kinyerezi Road,
Jumanne asubuhi

SIMULIZI YA RIZIKI

Riziki yetu ya kila siku hutoka kwa Mungu.
Simulizi kuhusu Riziki zasema kwamba Mwenyezi Mungu hutuma Malaika wake kila siku ili kuwafikishia Riziki zao Wanadamu wote.
Ili kupata Riziki yako ya siku yakupasa kuwepo pahala ulipopangiwa kupokelea Riziki yako ya siku hiyo kwa muda muafaka uliopangiwa pia.
Malaika wasipokukuta pahala ulipopangiwa katika muda huo, huirejesha Riziki hiyo kwa Mwenyezi Mungu.
Wengi wetu tumekuwa tunakosa Riziki kwa kutokuwepo pahala sahihi katika muda muafaka.
Ndiyo maana Binadamu, kila kukicha twakimbizana huku na kule. Yote hayo ni katika kubahatisha, Riziki yangu ya leo nitaipokelea wapi na wakati gani?

Saturday, November 4, 2017

KONGWA DUST RAIN

Mvua ya Vumbi maarufu Kongwa Rain Dust. Picha kutoka kwa mdau wa Blog yetu Dodoma, Ni maajabu ya Dodoma, 

SABATO YA VIJANA


Kutoka kwa wadau wa Blog Dodoma,
Tulikuwa na sabato njema na nzuri sana leo, sabato maalum ya watoto, baadhi leo wakitimishwa na kuhama madarasa, shalom akiwa mmoja wa wahitimu