Total Pageviews

Sunday, April 23, 2017

SUSY WILL BE LEAVING US

 
 
Ni dhahiri sasa Susy Nyanguli J. Kaigi anaicha Familia ya Kaigi kwa ajili ya kuanzisha familia mpya.
Jumapili, Flamingo Garden Inn
Tumekuwa na kikao kizuri cha maandalizi ya Kumuaga Suzy baadae mwishoni mwa Mwezi wa Saba mwaka huu.

PHOTO SHARING FROM BUNDA

 
 
 Baada ya Mapumziko ya Pasaka,
CK is back to school
Mbeza, Butiama
 
 
Nyamagoti mdogo,
Matumaini mapya.
Bunda, Jumapili

PHOTO SHARING FROM MUMBAI


Dr. George Msalya, who is in Mumbai India has recently shared photos with our Blog.
 Dr George anatoa ushuhuda:
"Mussa alipotumwa kwa Farao alikuwa na miaka 80,na akaongoza Israel kwa miaka 40, Blogger hajafikia hata 60........
Salem India ina wakazi zaidi ya Million kumi, Makanisa ya Sabato ni mawili tu yenye washiriki takribani mia moja.Mungu anatenda kazi, Sabato ya jana wamebatizwa watu 13"
 Itili,
Jasiri haachi asili
Chakula ughaibuni, ambacho huandaliwa kwenya jani la Mugomba.
Dosa
Katika jani la Mgomba pia.
Wanablog wanasema huu uaandaji wa chakula wa asili ni maarufu toka enzi na enzi kwa nchi za Afrika Mashariki. Tanzania, Rwanda na Uganda.

RIP THECLA ALFRED DADI

Safari yetu inatamalika hapa,
Makaburi Msafa, Mtwara.
Hapa amepumzika Mama yetu
Bi Thecla Alfred Dadi.
Akihitimisha safari yake ya Kidunia iliyoanza Mnyambe,Newala 1942.
Na sasa anasubiri pamoja nasi ufufuo kwa ajili ya Uzima wa Milele.

SABATO SDA MTWARA KATI

 Jumamosi,
Sabato katika Kanisa la Waadvensita Wasabato.Kanisa Mama Mtwara mjini.
Bw. Baruku akikutana na washiriki wengi waliopoteana muda sasa.
Kwa takribani miaka minne Baruku akihudumu hapa kama Mhazini wa Kanisa kabla ya kuhama hapa mnamo mwaka 2003.
 Msalya Tall katika darasa la Shule ya Sabato
 Kanisa Mama, Mtwara Kati
Bw Baruku anajivunia kuwa mshiriki mkubwa katika ujenzi wa Kanisa hili.
 Mzee Msalya,
Wazee wa Kanisa
Katika matangazo aliwasilisha salamu za Familia za Shukrani kwa washiriki wa Kanisa kwa namna ya pekee walivyoshiriki katika Msiba wa Mama yetu Thecla
 Mwinjilisti,
Kenedy Mshana
Katika mahubiri yake, yaliyojikita hadithi ya Daudi na Goliath alisisitiza sana Uinjilisti wa Vitabu
 
 
 
 Darasa la shule sabato,
Mageuzi makubwa ya kanisa la Sabato
Kusuka Nywele siyo tena jambo la kukutenga na kanisa
Bw Baruku ana ushuhuda kwamba kazi ya utume mjini Mtwara inaenda vyema.
Kutoka kanisa moja Mtwara mjini wakati wake hadi Makanisa Matatu sasa.

BACK TO MTWARA AFTER 34 YRS

Back in December,1983
Blogger, nikiwa Askari kijana R 3747aliyemaliza Mafunzo ya JKT, Oparesheni Safisha, Nachingwea wakati nikirejea kituo cha kazi Bagamoyo nilibahatika kupitia Mtwara. Mji uliokuwa ukifikika kwa shida kutokana na taabu ya usafiri.
Miezi michache kabla ya hapa, Mwanasheria Nyachiriga ndiyo alikuwa ameingia mjini hapa kuanza maisha kama Afisa wa Ardhi wa Upimaji.
Nilikaa Mtwara kwa takribani wiki moja hadi tulipopata usafiri wa kurejea Dar kwa MV Mapinduzi.
Pamoja na mipango mingi ya kutaka kutembelea Mtwara, haikuwezekana.
Lakini hatimae, baada ya miaka 34 kupita ninafanikiwa kurejea Mtwara kwa ajili ya kuja kuhani musiba wa mama yetu.
Ni safari ya kusisimua, yenye kuvuta Kumbukumbu za zamani.
Blogger, pamoja na uzee wa sasa najiandaa na Kamera mkononi kwa ajili ya kukuachia kumbukumbu.
Ni siku ya Ijumaa Kuu

 Temeke Sudan, mapema asubuhi kwa ajili ya kupata Tiketi za Safari.
Pamoja safarini ni wadau Baruku "Honda" na Msalya "Tall"
 Tunaabiri na Millenium Coach ya kuondoka Dar saa Tatu.
 
 
NANGURUKURU
Stop Over yetu, kwa ajili ya uchimbaji dawa na "Breakfast ya mchana"
Pahala maarufu kwa vitoweo vya samaki.........
Blogger Kamera mkononi
 
 
LINDI
Second stop Over.
Niliwahi kupita Lindi zamani.
Juni 1983, tukiwa on transit kuhamishwa Kambi za JKT nikitokea Ruvu kwenda Nachingwea.
Ni safari isiyosahaulika ya miaka hiyo,
Safari ya siku tatu kwa MV Lindi.
Lakini leo ni safari ya Masaa Manane na Millenium Coach
 Lindi bus Stand
 
Ming'oko
Bidhaa maarufu kusini.
 
Hatimae baada ya takribani masaa kumi njiani tunawasili Mtwara.
Mtwara ni moja ya miji jua linazama mapema.
Mnara wa Uhuru, unaobeba sasa pia nembo ya Ukimwi na Mnara wa mashujaa, Tanu Road ni Vitambulisho muhimu vya mji huu wa Mtwara ulio kusini mwa nchi yetu.