Total Pageviews

Thursday, June 4, 2015

HII NDIO AJALI ILIYOMUUA MPENDWA WETU JACKSON


Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa baada bas la kampuni ya Dar Lux likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na mistubishi fuso katika eneo la njia panda ya Berega wilaya ya Gairo barabara kuu ya Morogoro Dodoma.
Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Bonifas mbao amesema aliye fariki ni abiria aliye kuwa kwenye basi na chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa fuso alitaka kulipita gari jingine bila tahadhari na kusababisha ajali ya uso kwa uso.
 
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa fuso ambapo gari ilimshinda kutokana na utelezi katika eneo la Berega na kusababisha ajali hiyo.
 
SOURCE:

Wednesday, June 3, 2015

UTUMIAJI FURSA

Kuitumia Fursa,
Umeajiriwa Hospitali ya Muhimbili, kitengo chako Wadi ya wazazi.
Vitoto vinazaliwa kila siku, vinahitaji vijinguo kama vile visweta n.k.
Mama zao hawajawa na nguvu za kutosha kwenda kuwatafutia,
Hiyo ni fursa kwa Mkunga huyu....................
Duka la nguo za watoto litembealo mawadini.

BABA NA MAMA WAWILI

Baba na Mama wawili,
Muhimbili National Hospital on Sunday.
Mama wawili was discharged from Hospital yesterday afternoon.

HERE RESTS THE TWINS

Hakika Mungu hutenda kwa mapenzi yake,
Tarehe 28 May 2015 tukimshukuru Mungu na kumtukuza kwa mapenzi yake kwa kuwajalia Makubhi na mchumba wake watoto mapacha wa kiume, pamoja na kuzaliwa "Njiti" ilikuwa ni jambo lenye heri na baraka.
Pia tarehe hiyo hiyo akitujalia mtoto mwingine wa kiume kupitia kwa binti yetu Penina wa Nyang'oko, pamoja na kupatikana kwa njia ya upasuaji tunazidi kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Hata hivyo kwa wingi wa rehema zake,  na Mapenzi yake Mwenyezi Mungu aliamua tena kuwaita tena mapacha wake.
Doto (29.05.2015) baaada ya kuwa amepata matatizo ya upumuaji yaliyosababisha wakati mwingine kuwekwa kwenye mashine ya hewa.
na Kulwa (31.05.2015) baada ya matatizo ya kujaa gesi tumboni.

NI BWANA ALITOA, NA NI BWANA ALITWAA
JINA LAKE LIZIDI KUHUMIDIWA

KWAHERI JACK

Kwaheri Jackson Kaigi Marogo,
Ni vigumu kuamini, lakini ni vyema kukubali kuwa umetangulia....
Kwangu mimi hukuwa Mkwe tu, Ulikuwa ni Rafiki wa dhati, ndugu wa damu......
Bado naona kama ndoto tulivyokaa wote pale Samunge ukinipa ratiba yako ya safari,
Ndoto zako...............
Hata baadae wakati nikiangalia mpira pale Flamingo, sms yako iliponifikia, nikakupigia tukaongea tena.
Kuja kuambiwa baadae kuwa hauko nasi tena, ni jambo linaloumiza.
Tangulia, ni njia ya kila mja wake Mwenyezi Mungu.
Mapenzi yake Mwenyezi Mungu yatimizwe, Ni yeye alitoa na yeye ametwaa kilicho chake.
 KWAHERI
JACKSON KAIGI MAROGO
08.03.1962 - 31.05.2015