Total Pageviews

Wednesday, October 24, 2012

BONGO NA VIKWANGUA ANGA


  Ushirika Building
 Previously Nasaco offices 
 RITA, Makunganya

Ushirika, Lumumba
Vikwangua Anga kila uchao vinazidi kumea Bongo Darisalama
Ni vyema kuzuru jiji mara kwa mara.

MDAU KAONA

Bi Happy
Mdau wetu Silla kaona.
Na juzi jumapili akisindikizwa na wadau, akiwemo Chief Photographer walikwenda kujitambulisha.
Blogger ameachiwa kazi ya kupeleka "Kibanda".
Ni jambo la kheri, na Blog inawatakia kila la Kheri katika makusudio yenu wadau Silla & Happy


Friday, October 19, 2012

MACHWEO

Kunapokuchwa,
Hata Kunguru hurejea masikani kupumzika baada ya mihangaiko ya mchana kutwa.
Buguruni Shule, jana jioni

HII IMEKAAJE?

Hii imekaaje wadau?
Kwa wale waliopitia JKT, na mageshi mengineyo.....
Mwenye Rank kubwa anapaswa kukaa kulia.
Lakini sivyo kwa Askari hawa,
Sajenti na Mgambo nani zaidi?

Thursday, October 18, 2012

KWETU USWAZI

 
Kwetu Uswazi, huu ndio usafiri wetu wa kila siku.
Kinyerezi - Majumba Sita
Kinyerezi jana usiku

HEPIBETHIDEI YA MDAU NEEMA

 Msosi
 Vinywaji
 Keki
 Mdau Neema
Wadau wengi walihudhuria
Kama nilivyoahidi Blogger wenu nilihudhuria kuwawakilisha.

Wednesday, October 17, 2012

BLOG YAKO INA MUONEKANO MPYA

 
 
Blog yako sasa iko katika muonekano mpya.
Kutokana na mambo ya kitekinolojia yanavyozidi kubadilika,
Blog yako nayo imeamua kujivua gamba ililozaliwa nalo.
Hopefully utaipenda.
Na sasa kwa kila posts unaweza kuonyesha reaction yako.
Karibuni tuliendeleze libeneke la Blog yetu