Total Pageviews

Thursday, May 10, 2012

MAANDALIZI SEND OFF YA ROSE NYANDARO JOSEPH MAGWE

Vikao vinaendelea Rongai Bar, uwanja wa maonesho wa sabasaba
Jumamosi 07.05.2012 kilikuwa ni kikao cha nne
Baba Mzazi Joseph, Mwekahazina, Katibu na Mwenyekiti Mr Nyamwesa
Babu Mr Titus
Grace, Mbassa
Michango inaendelea kukusanywa
Send Off inatarajiwa ifanyike tarehe 22 June 2012 ukumbi wa Mgulani JKT

Wednesday, May 9, 2012

BONGO DARISALAMA, PAMOJA NA KADHIA YA KERO ZAKE PIA INA UNAFUU WAKE

Haki ya nani Ulimwengu una mambo yake,
na misemo yake kibao.
Utasikia
Ukiristo mgumu........
Uislamu mgumu............
Ujamaa mgumu.................
ama kweli
Na Bongo Darisalama nayo ngumu.
Mpaka Blogger anafikiria kuikimbia ifikapo 2020.
Lakini Bongo Darisalama si ngumu tunavyoiona wakati mwingine.....KAZI
Ukifanya kazi, Bongo Darisalama maisha yanaenda.
Dada ananunua vocha Zantel kwa mia 200, anabahatisha kuuza Special Numbers, akikupatia Tshs 1,800 zimeingia mfukoni, maisha yanaendelea
 Rafiki yangu mhaya, mtaalamu wa ushoni wa kuripea viatu, na ziada ya kukusanya chupa tupu za plastic, maisha yanaendelea pamoja na ulemavu wake. Na mchana si haba kumkuta AfriCentre akipata Safari moja ya moto na moja ya Baridi, na siku imepita.
Babu kwa kukusanya chupa tupu, hapa nilimkuta mitaa ya keko maliasili
 Bendera za timu za mpira, au za nchi mbalimbali zinamweka mjini mheshimiwa huyu
Reflectors za magari, Triangles, Jeki nk. hata kama hauzi kila siku
life goose on
Perfumes na airrefreshner, mitaa ya machinga complex Kawawa Rd
Benki za simu, MPESA, TIGO PESA, zote zinalipa
Mtaji wako unatosheleza? unayo leseni?
Bodaboda halali yako hata kama umejifunza asubuhi na jioni ukabeba abiria.
Bongo maisha yanaendelea

OFISINI LEO JUMATATU

Ofisini jumatatu 07.05.2012
Blogger kafikiwa na wageni wake.
Inshallah wageni wengine hakika hawana hata lepe la aibu.......
Chief Photographer kafika, kaona Camera mpya basi ikampata kazi ya kuanza kutupiga picha ofini mie na ma colleague wenzangu.
Nashukuru maana kupitia hapo nami nimepata kumbukumbu ya Blog yetu, ningepigwa lini picha ofisini mie. Ahsante Chief Photographer

Monday, May 7, 2012

ALMANUSURA ASUBUHI YA LEO

Vingunguti asubuhi ya leo,
Wadada wa skuli wako desparate hawajui usafiri wa shule watapata saa ngapi
Dakika chache baadae, karibu na CFAO Motors Daladala iliyokuwa mbele yetu tukaiona ikiacha barabara taratibu, almanusura iuparamie mti unaoonekana.