Total Pageviews
Wednesday, August 4, 2010
MSALYA: 1895 - 04 JUNE 1966
Wednesday, July 21, 2010
SIMULIZI ZA NAKATUBA COMING SOON
Thursday, June 3, 2010
FROM MWANZA TO NAKATUBA ON VEKESHENI
kwa mtiririko mzuri wa matukio, ni vyema ukaanza picha ya chini, kwa kupanda juu.
Sorry for Incovinience, ilitokana na matatizo ya kimtandao kidogo.
Naamini Vekesheni hii itabakia kumbukumbu safi kwa muda mrefu kwa vizazi vya kina Pricilla
Walikuja na Zawadi kibao.
Bi Penina alikuwa miongoni mwa waliojimwayamwaya na mizawadi kibao
Wenyeji walipopata nafasi, walikaa nakupumua kidogo............
Wakabadilishana mawazo.............
Maneno mazuri ya busara huwa hayakosekani wakati huo.

PLANNED NAKATUBA VEKESHENI
Wadau wamepania kufanikisha Vekesheni ya Nakatuba panapo mwezi wa Saba.
Mipangilio hii iwe babu kubwa kulikoni ile ya CK 55 yrs of nanihii.............
Hii ni ya Mwenyewe Dingi, Msalya Senior.
.............to 1966.
Hapa mdau mwakilishi wa Dar akijaribu kutayarisha itenerary ya safari nzima, ikiwa ni pamoja na ukadiriaji wa gharama za safari kwa ajili ya vekesheni hiyo.
Duh!!!
Wadau wametakiwa kuhakikisha wanajiandaa vilivyo,kwani kiasi cha chini cha kuweza kukamilisha Vekesheni yenyewe ni kama m4 kasoro ushee kidogo.
Lakini sina shaka, maana wadau wa kusini kule wamepania kikweli...
Na central nako ndio usiseme.
Lazima twende pamoja
Monday, March 8, 2010
KUMBUKUMBU YA VEKESHENI

Katika kupitia pitia nikakutana na picha ya zamani zile...
Ilikuwa kama Vekesheni vile.
Ilikuwa safari ya Nakatuba,
Dada mmoja anajiandaa kupata Mwenza.........
Tukasema tukampe Kampani
Hapa tunakaribia kijijini, tukaambizana maji yetu haya ya kizungu kizungu hayafai huko vijijini, hivyo tupige mafunda mawili chap chap tuanze.
Chupa itawafaa kwa kuchukulia mafuta ya Taa.
Ni pale kilima cha Manana.
Enzi tunakua, thubutu kama kulikuwa na mtu ana ubavu wa kufika hapa na kupumzika vile na kupiga picha.
Kuanzia shoto Blogger mwenyewe, Penina na Lulu
SIMULIZI ZA MZEE CK NA UKOO WA MSALYA

Simulizi hii inaanzia karibu miaka 200 iliyopita………………….
Hii imetoholewa kizazi kwenda kizazi na Bw. Seka Seka, na dadie Nyabhwangu Kisaka.
Simulizi inasema hivi
Zamani hizo, karibu miaka 200 iliyopita,
Bw. Manyori aliyekuwa akiishi sehemu za Sizaki alielekea sehemu za Bukwaya.
Huko Bukwaya Manyori alijaaliwa kukutana na Binti mmoja, ambae alikuja kuwa mke wake.
Jina hili limepotea kwenye kumbukumbu za msimuliaji.
Manyori na huyu mama kwa kumbukumbu zilizopo, walifanikiwa kupata watoto.
Idadi ya watoto hakuna uhakika sana, lakini watoto wawili wa kiume ambao kumbukumbu zipo ni Bw. Kisaka (Chisaka) na Kimori (Chimori).
Ukoo ukaendelea
Kisaka akamzaa Nyabhwangu na Nyesagi (mabinti hawa) kwa mkewe Mkoko
Kimori akamzaa Maseeme.
Miaka ikapita, Mzee Kisaka akafariki. Kwa taratibu za mila Bw. Maseme akaruhusiwa kumrithi mke wa Kisaka (Baba yake mkubwa), Bi Mkoko au Nyakagere.
Maseme kwa mke wa Kisaka(Bi Mkoko) wakawazaa Msalya na Nyalimbi.
Hebu tutafakari hapa kidogo,
Nyabhwangu na Maseme ni Dada na Kaka (kwa baba mkubwa na mdogo)
Msalya na Nyalimbi ni wadogo zake na Nyabhwangu (mama mmoja)
Msalya na Nyalimbi wanae Maseme (Hakika damu yake)
…………basi pia Nyabhwangu ni shangazi yake Msalya………….
Maisha yanaendelea ukoo unaendelea
Maseme alifariki akimwacha Msalya akinyonya, Mama yake na Msalya baada ya kifo cha mumewe, alihama kutoka Bukwaya kwenda kuishi sehemu za Kisorya eneo la Nambubhi. Enzi hizo ikiwa katika utawala wa Ukerewe, wilaya ya Mwanza mkoa wa Lake Province.
Lake Province sasa ndiyo Kagera, Shinyanga, Mwanza na Mara kwa pamoja.
Nyabhwangu kwa mume wa kwanza wa Ukerewe akamzaa Mnyaga.
Baadae kwa mume wa pili wa Kiruli akawazaa Manoko, Muruguta na Nyamakale.
Nyalimbi akawazaa Kalyanja, Nyamumwi na Nyanyama
Msalya kwa wakeze tofauti akawazaa Bhajalaki, Manyori, Kurwijira, Mwayai, Nyanjula, Gabhaseki, Chabhusiku, na Taabu.
Msalya aliishi na kukulia Kisorya Nambhubi. Watoto Bhajalaki, Manyori, Kurwijira, Mwayai, Nyanjula wamezaliwa hapo. Baadae kwenye mwaka 1937 alihama kuelekea Kitengule, eneo panapojulikana zaidi sasa kama Nyakatubha. Hapa ndipo watoto wake Gabhaseki, Chabhusiku, na Taabu walizaliwa. Msalya alikaa eneo hili hadi alipofariki mwaka 1966.
Kwa upande wa pili, Bibi (Nyanya) yake Msalya alitokea Kisiwa cha Ukara, akaolewa huko maeneo ya Bukwaya na Bw. Kagele. Miongoni mwa watoto wao ni Binti yao aliyeitwa Mkoko (jina la kuzaliwa) lakini akijulikana zaidi kama Nyakagele kwa kutumia jina la Baba.
Kumbukumbu zinazopatikana, Kagele amezaliwa pamoja na Kaka yake akiitwa Kwesi na akiwa na mdogo wake akiitwa Lugeji.
Kwesi akamzaa Mgole.
Mgole akiishi pale eneo la Kasahunga nae akawazaa Kwesi na Mkwaji.
Kwesi Mdogo akimzaa Mkumbya, Ebunda, Kagere, Lyanga na wadogo zao wa kike.
Lugeji hakubahatika kupata motto.
Next time nitawaletea matawi yanayoendelea
Family tree…………………………

Subscribe to:
Comments (Atom)